tiko
tiko
Matukio ya mauaji ya kikatili dhidi ya wanawake katika wilaya ya Butiama yameanza
kurejea upya baada ya mwanamke mmoja mkazi wa kijiji
cha Maneke katika halmashauri ya Musoma mkoani Mara kuuawa
kinyama kwa kukatwa mapanga
tukio ambalo limehusishwa na imani za kishirikina.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Mara kamishna msaidizi wa jeshi la polisi ACP Philip Alex
kalangi, amesema kuwa mwanamke huyo Mwadawa Elias mkazi wa
kijiji hicho cha Maneke, ameuawa baada ya kuvamiwa akiwa
amelala nyumbani kwake majira ya usiku na watu zaidi
ya wanne kisha kuanza kumshambulia kwa kumkata
kata kwa mapanga.
Mwanzoni mwa mwaka jana zaidi ya wanawake 40 katika tarafa ya Nyanja wilaya ya Butiama waliuawa kinyama kwa kuchinjwa na wengine kukatwa mapanga kisha
wauaji kuchukua baadhi ya viungo
vya miili ya marehemu kwa imani hizo za ushirikina na
kusababisha hofu kubwa kwa jamii katika eneo hilo
kabla ya hatua mbalimbali kuchukuliwa na serikali kupitia
vyombo vyake vya dola katika kudhibiti ukatili huo.
tiko
tiko
Post a Comment