tiko
tiko
MADEREVA Daladala jijini Arusha,leo
wamefanya mgomo wa kutoa huduma ya kusafirisha abiria katika maeneo
mbalimbali ya jiji hilo kwa kile kinachodaiwa kugomea kuanzishwa kwa
safari mpya wanayotakiwa kuianza hivi sasa.
Wakazi wa maeneo mengi ya jiji hilo
wanalazimika kutembea kwa miguu, huku wengine wenye uwezo kidogo
wakitumia usafiri wa bodaboda ili kuwahi katika shughuli zao za
kuendelea kujitafutia chochote. Askari Polisi na Wanamgambo wamesambaa
kila kona jijini Arusha.
Safari zenye mgogoro zaidi ni zile za Kutoka Njiro na Moshono kuelekea mjini.
tiko
tiko
Post a Comment