tiko
tiko
MIKEL RUFFINELLI ndiye
mwanamke mwenye ‘mahips’ (nyonga au makalio) makubwa zaidi duniani hivi
sasa na ameingia katika Kitabu cha Kumbukumbu za Dunia cha Guinness.
Mama huyo ambaye ni Mmarekani, anasema anajisikia raha mustarehe na umbo lake hilo alilo nalo.
Ruffinelli ambaye ni mama wa watoto wanne, mkazi wa Jimbo la California, Marekani, anasema anaishi maisha ya kawaida na kuendesha kazi zake vizuri ambapo mumewe, Reggie Brooks, pia humsifia kwamba anampenda jinsi alivyoumbika.

Kwa mujibu wa gazeti la ‘WorldWide Werid News’, Ruffinelli alikuwa na
umbo la kawaida kabisa wakati wa ujana na hakuwa na tatizo lolote la
kuongezeka uzito, lakini, akiwa na umri wa miaka 22, alianza kuona
‘mahips’ yake yanazidi kuongezeka baada ya kuzaa mtoto wake wa kwanza.
Aliongeza kusema kwamba kila alipokuwa anazaa, sehemu yake hiyo ya mwili
ilizidi kuongezeka mpaka akawa anashindwa kupita kwenye mlango wa
kawaida. Japokuwa kiuno chake kina inchi 40 (sentimita 102), nyonga
zake zinafikia inchi 100 (sentimita 254), hali inayomfanya avunje rekodi
ya dunia.
Pamoja
na kwamba watu humshangaa kila anapopita na humwomba kupiga naye picha
za kawaida na za video kutokana na umbo lake hilo, bado hujisikia mwenye
furaha.
Anasema: “Ninapotembea mitaani, watu hunipiga picha za kawaida na za
video kutoka kwenye simu zao. Watu wengine hufikiri kwamba nilifanyiwa
upasuaji ili kuupa mwonekano wa kupendeza mwili wangu, lakini ukweli ni
kwamba umbo hili ni la asili.”
Ruffinelli hana mpango wa kupunguza unene wake, lakini anakiri kwamba
umbo lake hilo humfanya nyakati fulani akate tiketi za viti viwili
anaposafiri kwenye ndege, kwani kiti kimoja hakimtoshi.
Umbo lake humlazimu kupita kiubavu katika milango mbalimbali na huwa hawezi kufunga mlango wa bafu lake wakati akioga kwani sehemu ya mwili wake huwa imejitokeza nje.
Umbo lake humlazimu kupita kiubavu katika milango mbalimbali na huwa hawezi kufunga mlango wa bafu lake wakati akioga kwani sehemu ya mwili wake huwa imejitokeza nje.
tiko
tiko
Post a Comment