tiko
tiko
HOFU! Waigizaji
wa tasnia ya filamu Tanzania, ambao walikuwa wameanza kusahausahau
misiba mfululizo iliyowatokea miaka michache iliyopita, juzikati
walijikuta wakitoneshwa kidonda, baada ya kutokea kifo cha muigizaji
Tino Madhahabu, kilichotokea Tunduma mkoani Mbeya, kufuatia kuugua kwa
muda mrefu.
Msanii huyo aliyetamba katika uigizaji
akiwa na Dude katika kipindi maarufu cha Bongo Dar es Salaam, kwa muda
wa miaka saba na baadaye kuingia kwenye filamu alikuwa akiugua ugonjwa
wa moyo, kiasi cha kumfanya arejee nyumbani kwao kwa ajili ya matibabu,
ambayo hata hivyo, yameshindwa kunusuru uhai wake.
Kifo hicho kimeibua hofu upya kwa
wasanii wa Bongo Muvi, hasa ikikumbukwa kuwa mchunguji mmoja (jina
tunalihifadhi) aliwahi kutabiri kuwa, wimbi hilo la vifo litaendelea
tena mwaka huu kwa wasanii na watu wengine maarufu, wakiwemo wanasiasa
hivyo kuwataka kumrudia Mungu.
Wasanii kadhaa waliozungumza na Ijumaa
baada ya taarifa za msiba huo walionesha hofu ya kifo waliyonayo lakini
wengi wakasema Kifo cha Tino ni mipango ya Mungu hivyo kila mmoja
ajiandae tu.
Msanii aliyewahi kufanya kazi kwa karibu na Tino, Kulwa Kikumba ‘Dude’ alisema: “ Dah! Ni kweli jamaa katutoka, kikubwa tumuombee na hilo la hofu ni vyema kila mmoja akawa nayo ili aweze kujiandaa kwa safari.”

Msanii wa filamu Bongo, Devota Mbaga.
Katika kuonesha kuweweseka, msanii
mwingine wa filamu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ alisema: “Mimi sitakufa
kwa kuwa niko karibu na Mungu, watakaokufa ni wale walio mbali na
Mungu.”
Msanii mwingine, Isabela alisema kifo cha Tino kimemshtua mno na kusema ni mapenzi ya Mungu, lakini akaponda utabiri wa mchungaji akisema hajawahi kuamini mambo hayo, kauli ambayo pia ilitolewa na Rose Ndauka.

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni,
kulikuwa hakuna taarifa rasmi zilizotolewa juu ya mazishi ya msanii
huyo.Mungu Ilaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina- Mhariri
Imeandikwa na Hamida Hassan, Gladness Mallya na Deogratius Mongela.
Imeandikwa na Hamida Hassan, Gladness Mallya na Deogratius Mongela.
tiko
tiko
Post a Comment