tiko
tiko
Jeshi
la polisi mkoani singida limekamata risasi miambili sabini na moja za
bunduki ya kivita aina ya SMG, zilizo kuwa kipelekwa wilayani manyoni
kwa ajili ya kufanyia uhalifu.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa singida ACP Thobias Sedoyeka amemtaja aliye
kutwa na risasi hizo baada ya polisi kuweka mtego katika kituo cha
mabasi cha wilyani manyoni, ni bwana Discon Bavumbi Masombo Kiyungu
mkulima na mkazi wa matele wilaya ya kasulu mkoani kigoma,anayesadikiwa
kutokanazo nchi ya burundi na kuzipeleka porini kwa ajili ya
kuwindia tembo na kufanya ujangili mwingine.
Katika
tukio lingine kamanda Sedoyeka amesema mwanafunzi Frida Ibrahimu
miaka kumi wa darasa la nne katika shule ya msingi kamenyanga wilyani
manyoni amegongwa na kufa baada ya dereva mgana msumbe ayekuwa
akiendesha gari lenye usajili wa namba t 740 skl aliyekuwa akitoke
dodoma na kuelekea singida kumgonga mtoto huyo.
Katika
tukio la kwanza la kukutwa na risasi kinyume na sheria mtuhumiwa
anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi ili kubaini mtandao
mzima na kupata bunduki ambayo inatumia risasi hizo,pia katika tukio la
pili kamnda sedoyeka amewataka watumiaji wote wa barara kuzingatia
sheria ili kupunguza vifo ambavyo siyo vya msingi.
tiko
tiko
Post a Comment