Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

Nimekuletea taarifa hii ya matumaini kwa watu wa Mali kuhusu Ugonjwa wa Ebola

tiko tiko
ebola_3022684bMwaka 2014 haukuwa mwaka wenye story nzuri kutoka nchi za Afrika Magharibi kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola watu zaidi ya elfu kumi walifariki na wengine zaidi ya elfu tano wakiripotiwa kuugua ugonjwa huo.
Umoja ya Mataifa na Serikali ya Mali wametangaza kuwa nchi hiyo haina tena ugonjwa hatari  wa Ebola baada ya kutoripotiwa taarifa za mgonjwa yeyote wa Ebola kwa muda wa siku kipindi cha siku 42 zilizopita.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na Ebola ulioandikwa katika ukurasa wa Twitter unawashukuru wafanyakazi wa Afya waliojitolea kupambana na Ebola nchini Mali kwa kuhakikisha ugonjwa huo umedhibitiwa.
Mbali na Mali kuonekana kuathiriwa na ugonjwa huo, Guinea, Sierra leone na Liberia ni mataifa ambayo yamepata athari kubwa kutokana na ugonjwa huo.
Waziri wa Afya wa Mali amewasifu wahudumu wa Afya  na washirika wa Kimataifa kwa msaada wao.
Nimekurekodia taarifa hiyo kwenye kituo cha WBS unaweza kuisikiliza hapa.
Hakuna Story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitiatwitter, instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top