Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

Bill Gates kwenye huu mradi wa maji yanayotokana na taka za binadamu!

tiko tiko
gateMmiliki wa kampuni ya Microsoft Corporation, Bill Gates ameendelea kuuthibitishia ulimwengu kwamba haogopi kuwekeza pesa yake kwenye biashara yoyote Duniani.
Ni mmoja ya watu wanaofadhili miradi mikubwa ya kilimo Afrika, leo kuna hii story ambayo kama ingekuwa Bongo mtu anawekeza upande huu ni wachache ambao wangemuunga mkono.
Picha na video zimeenea mitandaoni, Gates kaamua kugeukia huu mradi wa maji safi ya kunywa ambayo yametengenezwa kutokana na kinyesi cha binadamu.
Mikakati ya Gates ni kushirikiana na Kampuni hiyo kusambaza mitambo hiyo katika nchi mbalimbali maskini ikiwemo Senegal muda mfupi baada ya majaribio yake kukamilika.
Teknolojia hiyo imeungwa mkono na shirika la WaterAid ambalo limesema kuwa litasaidia sana katika maeneo ya mengi yenye ukame ambapo kulingana na shirika hilo watu millioni 748 hawana maji safi ya kunywa.
human
Video iliyowekwa katika blog yake, Bill Gates alishuhudia hatua zote, kuanzia kinyesi cha binadamu kikiingizwa katika mtambo huo mpaka maji yalipotoka na akayanywa baada ya kupitia hatua zote za utayarishaji.
Cheki video hii inayoonyesha mfumo mzima wa maji hayo yanavyoandaliwa kutoka kwenye mfumo wa taka.

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top