tiko
tiko
Kaseja
ambaye amekuwa kwenye mgogoro wa malipo ya fedha za usajili na uongozi
wa Yanga mpaka akafikia hatua ya kugoma kufanya mazoezi na timu hiyo
wakati wa uongozi wa kocha Marcio Maximo,
leo hii klabu ya Yanga imeamua rasmi kukata mzizi wa fitna na kumuacha
mchezaji huyo waliyemsajili msimu uliopita baada ya kuachwa na Simba.
Akizungumza mjini hapa, Mkurugenzi wa Habari wa Yanga, Jerry Muro amesema Kaseja amevunja mkataba kutokana na kutokwenda mazoezini kwa saa 48.
“Kaseja haidai Yanga na fedha zake aliishalipwa, tarehe zinaonyesha siku fedha hizo zilipolipwa“– Jerry Muro.
“Pia
katika mkataba hakukuwa na sehemu inaonyesha ni lazima Kaseja alipwe
siku fulani lakini ilikuwa ni lazima alipwe ndani ya kipindi cha mkataba“– Jerry.
“Yeye
aliamua kususa kuja kazini, jambo ambalo lilivunja mkataba wake na
Yanga… Kwa kuwa hatudai, tumeona ni vema kumuachia aende aendako na
tunamtakia kila la kheri kama klabu ya Yanga,” alisema Muro“– Jerry Muro.
Muro pia amesema Kaseja alianza kuwa na kinyongo na Yanga baada ya benchi la ufundi kuanza kumtumia Dida kutokana na kuwa na uwezo zaidi kumzidi kwakuwa katika mechi zilizopita alionekana kushindwa kumudu.
Nitakufikishia kila stori inayonifikia
mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram
na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment