tiko
tiko
Kingunge Ngombale Mwilu.
Heshima yako mzee! Najua una mambo mengi
ya kufanya, ukichanganya na umri wako, itakuwa vigumu sana kwa mtu kama
mimi kuonana ana kwa ana na wewe. Hiyo ndiyo sababu iliyonifanya niamue
kutumia ukurasa huu kufikisha ujumbe wangu kwako.
Mheshimiwa, mimi si mwanasiasa mkongwe
kama wewe ambaye umeitumikia nchi hii tangu enzi za Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere mpaka leo hii. Sijawahi kushika nyadhifa mbalimbali
kwenye nchi hii, zikiwemo ukuu wa mikoa kadhaa, ubunge wala uwaziri.
Wala sijawahi kuwa mwanaharakati wa kusimamia ujamaa kama wewe.
Sijui chochote kuhusu siasa, utawala
wala historia ya nchi hii, niponipo tu, kama bendera inayofuata upepo.
Hata hivyo, ningekuwa mimi kwenye nafasi yako, nakuhakikishia mzee
nisingefumbua mdomo wangu kuwananga wote waliojitokeza kuwania urais
kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) bila kwanza kujifanyia tathmini mimi
mwenyewe juu ya uadilifu wangu.
Kila mtu anao uhuru wa kuzungumza mawazo
yake hadharani, naamini na wewe uliitumia vyema haki yako hiyo ya
kikatiba, hivi karibuni ulipoonekana na kusikika kupitia kituo kimoja
cha runinga ukisema wote waliojitokeza kuwania nafasi hiyo hawana sifa
kwa kuwa wanatumia fedha kutaka kuingia ikulu.
Sipingi ulichokisema, ni kweli kwa kipindi kirefu imekuwa ni kawaida ya wanasiasa au watawala waliopo madarakani, kutumia fedha kama njia ya mkato ya kuwafanya wapate nafasi za juu za uongozi, hilo liko wazi na hakuna asiyelijua.
Sipingi ulichokisema, ni kweli kwa kipindi kirefu imekuwa ni kawaida ya wanasiasa au watawala waliopo madarakani, kutumia fedha kama njia ya mkato ya kuwafanya wapate nafasi za juu za uongozi, hilo liko wazi na hakuna asiyelijua.
Kinachonishangaza, kwa nini kauli yako
hiyo ije leo? Mheshimiwa, umekuwa kwenye siasa kwa kipindi kirefu sana,
umeona mengi na naamini hata hili ulilolisema hivi karibuni, ulikuwa
ukilijua kwa kipindi kirefu na kwa namna moja au nyingine ulikuwa
ukiliunga mkono ndiyo maana licha ya kushika nyadhifa nyingi kubwa
kwenye taifa hili, hujawahi kuisaidia serikali kupambana na viongozi wa
aina hiyo.
Kama nimesahau nikumbushe mzee, ni lini
ulipoisaidia au kuishauri Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa
(Takukuru) au jeshi la polisi kuwanasa watu wa aina hiyo? Kama hujawahi
kufanya hivyo wakati ulikuwa unajua faulo zilizokuwa zikichezeka kwa
kipindi kirefu, basi na wewe ni miongoni mwa wacheza faulo.
Ndiyo! Licha ya mchango wako mkubwa
katika siasa za nchi hii, misimamo yako inatia shaka mzee. Kabla ya
uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Kanisa Katoliki Tanzania lilitoa waraka wa
kuwaelekeza waumini wake kuwa makini na wanasiasa waliokuwa wakiwania
nafasi mbalimbali za uongozi na kuwataka kutowapa nafasi viongozi
wanaoendekeza rushwa na kusahau matatizo ya wananchi.
Mzee, wewe ulikuwa miongoni mwa watu
walioupinga vikali waraka huo, ukaingia kwenye malumbano makubwa na
viongozi wa kidini, umesahau? Kwamba kitendo cha kanisa kuwatahadharisha
waumini wake kutowachagua wala rushwa kilikukera sana. Leo na wewe
unazungumza kitu kilekile, kipi kilichokufanya ubadilike na kuwa na
misimamo isiyoeleweka?
Watanzania bado hawajasahau jinsi
familia yako ilivyohusishwa na kampuni ya kukusanya ushuru kwenye Stendi
ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya Ubungo (Ubungo Bus Terminal),
iliyoisababishia serikali upotevu wa mabilioni ya shilingi.
Historia yako inakuhukumu mzee, ingekuwa
vyema kama ungejitathmini kwanza kabla ya kutoa kauli hiyo kwa sababu
inawafanya wengi washindwe kukutafsiri unasimamia upande gani.
Wasalaam.
Wasalaam.
tiko
tiko
Post a Comment