Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

Story za alichosema Baba wa Beyonce kuhusu kufilisika… Safari ya Jay Z na Beyonce Thailand

tiko tiko
beyonce-and-mathewKulikuwa na story mitandaoni ambazo hazikuwa nzuri kwa familia ya mzee Mathew Knowles, ikasemekana eti amefilisika mpaka kafikia hatua ya kuuza vitu mbalimbali ikiwemo nguo za watoto wake, yaani Solange na Beyonce pamoja na CD za nyimbo za Bey.
Hii haikuwa taarifa nzuri, Beyonce kaongoza kwa kuingiza pesa nyingi upate wa mastaa wa kike Marekani, ina maana amemtelekeza Baba yake?
Mzee Knowles amekanusha story hizo; “Ningehitaji pesa nisingeuza T-shirt ya dola 5, ningeuza tuzo ya Grammy au BET…
beyonce-garage-sale-jpg
Mzee huyo kasema anauza vitu hivyo ili kupunguza mlundikano wa vitu ambavyo vilikuwa vinajaza nafasi tu ndani ya jengo la ofisi yake ambayo anapanga kuikarabati upya mwakka 2015.
Kwa hesabu ya haraka haraka ya vitu anavyoviuza Mzee Knowlese ni kama atapata dola 2000/= tu.
Hayo yanaendelea Marekani, lakini Beyonce yuko na familia yake, Jay Z na mtoto wao Blue Ivy maeneo ya Thailand, picha za mwisho wameshare wakiwa kwenye ukumbi mkubwa wa Michezo wa  Muay Thai wakiangalia mchezo wa ngumi.
Jay Z iii Jay Z
Hapa kuna video inayoonyesha Mzee Knowles akiendelea na mauzo ya vitu hivyo.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top