Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

Ester Kiama: Nammeneji Tu Dude Wala Si Mchepuko Wake

tiko tiko
Ester Kiama: Nammeneji Tu Dude Wala Si Mchepuko Wake
Baada minong’ono kuzagaa kila kona kuwa kuna uhusiano wa kimapenzi kati ya mwigizaji wa kike Ester Kiama na muongozaji na mwigizaji Kulwa Kikumba, mwanadada huyo amekanusha na kudai kuwa yeye ni meneja tu wa msanii huyo na anamsimamia kurudisha Bongo Dar es salaam.
Kweli nipo karibu sana na Dude kikazi na si kimapenzi kama wengine wanavyofikiria, nammeneji tu katika uwezeshaji wa kurudisha kipindi chake cha Bongo Dar es Salaam na masuala ya filamu, tumerekodi sinema yangu ya Ngoma ngumu,”anasema Ester.
Akizungumza na FC  Dude naye aliungana na mwanadada huyo kuwa ni meneja wake na wana malengo ya kufanya makubwa naye hawezi kufanya ujinga huo kwani ana familia yake anayoiheshimu na hawezi kumsaliti mkewe Eva anampenda sana, na masuala ya kazi tu, hakuna mapenzi.
“Ester kwa sasa ni meneja wangu wala sina uhusiano naye nipo naye kikazi na ndio meneja wangu kwa sasa katika kazi zangu za kisanaa katika filamu na Bongo Dar es Salaam,”anasema Dude.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top