tiko
tiko
Bidhaa za vyakula katika moja ya masoko nchini. Picha ya mtandao.
Upungufu
wa chakula kwa baadhi ya mikoa nchini umeendelea kusababisha ongezeko
la mfumuko wa bei wa Taifa kutoka asilimia 4.2 hadi asilimia 4.2 ndani
ya mwezi mmoja.
Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii kutoka
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraimu Kwesigabo, aliwaambia waandishi
wa habari leo kuwa, kutokana na upungufu huo bei za bidhaa za vyakula
zimeongezeka.
“Mfumuko wa bei wa Taifa kwa kipimo cha
mwaka unapimwa kwa kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na
huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi,”alisema.
Aliongeza: “Hivyo kutokana na ongezeko
la bei za bidhaa hizo pamoja na huduma zote kwa kaya zimesababisha
mfumuko wa bei wa taifa,”alisema Kwesigabo.
Aliendelea kueleza kuwa, kasi ya
upandaji wa bei za bidhaa hizo zimesababisha mfumuko wa bei wa Taifa kwa
mwezi iliyopita kuongezeka hadi ukufikia asilimia 4.3 kutoka asilimia
4.2 ya mwezi Februari mwaka huu.
Kwesigabo alisema, ongezeko la mfumuko
wa bei kwa mwezi Machi umesababishwa hasa na kuongezeka bei za bidhaa za
vyakula kwa kipindi kilichoishia Machi mwaka huu tofauti na ilivyokuwa
kwa Machi mwaka jana.
Alizitaja bidhaa hizo kuwa ni pamoja na mchele, unga wa muhogo, nyama, samaki, maharage, choroko na sukari.
Alisema kutokana na hali hiyo wananchi
wataendelea kushuhudia bei za vyakula zikiendelea kupanda na kwamba bei
waliyokuwa wakinunua bidhaa za vyakula hapo awali itabadilika.
Akizungumzia thamani ya shilingi ya
Tanzania kwa mwezi uliopita ikilinganishwa na mwezi Septemba, 2010
alisema, uwezo wa Sh 100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia Sh 64
na senti 15 mwezi Machi mwaka huu kutoka Septemba, 2010.
“…ikilinganishwa na Sh 64 na senti 59 ilivyokuwa Febriari mwaka huu,”alisema Kwesigabo.
tiko
tiko
Post a Comment