tiko
tiko
Duh! Kama
ulikuwa unaamini kuwa lile bifu la wakali wawili wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Saleh Kiba, limekwisha, basi umenoa
baada ya jamaa hao kukutana ukumbini na kuchuniana.
Ishu hiyo ilijiri kwenye Ukumbi wa
Hoteli ya Double Tree Hilton jijini Dar, juzikati ambapo wasanii
mbalimbali walikutanishwa na kampuni moja ya huduma ya simu za mkononi
ili kuzungumza na wanahabari juu ya maandalizi ya tamasha.
Waandishi wetu, wakiwa wameingiwa na
roho ya kutaka ‘ubuyu’, hatimaye muda wa kuingia Kiba ukawadia ambapo
alitinga na timu yake ya watu wanne.
Alipofika, Kiba alikaa sehemu ya viti vya kushoto akiwa bize na mrembo mmoja wakichati kabla ya Diamond kutimba na timu yake kubwa.
Alipofika, Kiba alikaa sehemu ya viti vya kushoto akiwa bize na mrembo mmoja wakichati kabla ya Diamond kutimba na timu yake kubwa.
Kama ilivyo ada, macho ya waandishi wetu
yakaelekezwa kwa Diamond huku mapichapicha yakiendelea kwa ajili ya
kutupia kwenye mitandao ya kijamii.
Kila msanii aliyefika kwenye ukumbi huo alianza kutoa salamu kwa mtu anayeona anafaa kwake, lakini cha kushangaza mastaa wawili Kiba na Diamond walishindwa kupeana hata mikono huku kila mmoja akiwa ameuchuna na kampani yake.

Hata hivyo, wakati ulipofika wa wasanii
kujitambulisha mbele ya wadau, mastaa hao walitahadharishwa kwamba
atakayeanza au atakayekuwa wa mwisho kujitambulisha haina maana kwamba
yeye ndiye mkubwa zaidi kistaa.
Katika kujitambusha, Kiba ndiye aliyeanza huku kila mtu akitamba kufanya vizuri kwenye kila shoo zitakazofanyika mwaka huu.Hakuna aliyekuwa tayari kumzungumzia mwenzake.
tiko
tiko
Post a Comment