tiko
tiko
STAA aliyewahi
kukamata vilivyo kwenye anga ya muziki wa Bongo Fleva, Shabani
Ramadhani ‘Matonya’ ameibuka na kumvaa mwanadada Judith Wambura ‘Jide au
Lady Jaydee’ akidai amemdhalilisha kwa mashabiki wake.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Matonya
alisema anamtafuta Jide popote alipo ili amuulize kinaga ubaga kwa nini
aliamua kuposti picha kwenye mitandao yake ya kijamii ikimuonesha akiwa
hajitambui pasipo kumtaarifu.
“Nimeumizwa sana na Jide kwa kitendo
chake cha kuamua kunidhalilisha kwa kiasi hicho tena akijua mimi ni
mwanamuziki mwenzake na kama kuna kitu aliona simfurahishi kwenye
mwenendo wa maisha yangu basi alikuwa wazi kuniita na kunikalisha chini
na siyo kama uamuzi alioutumia wa kunianika kwenye mitandao,” alisema
Matonya.
Matonya alifafanua kuwa picha hiyo
alipigwa katika video yake mpya lakini Jide akaichukua na kuiweka
mitandaoni pasipo kumuuliza.
Matonya akiwa mtungi.
“Ile picha aliyoitumia kunidhalilisha
ilikuwa ni ya video yangu ya wimbo mpya unaoitwa Homa ya Jiji ambayo
itatoka hivi karibuni, sasa yeye ameweka mitandaoni na kusababisha watu
wanidharau kwa kuona nimelewa chakari, asiponiomba radhi nitahakikisha
namfikisha mahakamani,” alisema Matonya.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Jide
aliiposti picha ya Matonya akiwa amelala na kusindikiza na ujumbe
ulioonesha kama hamjui msanii huyo hali iliyosababisha mashabiki wengi
kumsema vibaya Matonya.
tiko
tiko
Post a Comment