tiko
tiko
Baraza
la Mitihani la Taifa nchini Tanzania NECTA leo limetoa matokeo ya
mtihani wa Taifa wa Kidato cha pili mwaka 2014 kwa wanafunzi waliofanya
mtihani huo unaowapa fursa ya kuendelea na kidato cha tatu.
Akisoma
taarifa hiyo leo kwa waandishi wa habari katika ofisi za NECTA jijini
DSM, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema kiwango
cha ufaulu kwa mwaka 2014 kimeongezeka kwa asilimia 3.32 kutoka asilimia
89.34 mwaka 2013 hadi asilimia 92.66 mwaka 2014.
Amesema
waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 453,191 lakini waliofanya
mtihani walikuwa 405,204 sawa na asilimia 89.40 na kwamba wanafunzi
47,987 sawa na asilimia 10.60 hawakufanya mtihani huo kwa sababu
tofauti.
Dkt
Msonde amesema Jumla ya wanafunzi waliofaulu kwa kupata alama
zinazowaruhusu kujiunga na kidato cha Tatu ni 375,434 sawa na asilimia
92.66 ambapo kati yao wasichana ni 195,328 na wavulana ni 180,106.
Jumla
ya wanafunzi 29,770 sawa na asilimia 7.34 wamefeli kwa kushindwa
kufaulu kwa kiwango kinachotakiwa, na hivyo watalazimika kukariri
darasa.
Dkt
Msonde amesema kuwa matokeo hayo yamepangwa kwa mfumo Wastani wa Pointi
(GPA) ambapo madaraja yamepangwa kwa Distinction, Merit, Credit, Pass
na Fail.
Jumla ya wanafunzi 180,965 sawa na asilimia 44.66 wamefaulu kwa madaraja ya juu (Distinction, Merit na Credit).
Ametaja ufaulu kwa kila daraja kuwa ni kama ifuatavyo
Distinction wanafunzi 35,656 sawa na asilimia 8.8
Merit wanafunzi 57,945 sawa na asilimia 14.30
Credit wanafunzi 87,364 sawa na asilimia 21.56
Pass wanafunzi 469 sawa na asilimia 47.99.
Kwa
upande wa ufaulu katika masomo, Dkt Msonde amesema kuwa somo
lililoongoza kwa ufaulu ni History ambalo wamefaulu kwa asilimia 90.71
na somo lenye ufaulu mdogo zaidi ni Basic Mathematics ambalo ufaulu wake
ni asilimia 18.15.
Masomo
yenye ufaulu mzuri ni Civis, History, Kiswahili na English ambapo
ufaulu ni asilimia 84 yakifuatiwa na Geography, Biology na Book-keeping
yenye ufaulu wa kati ya asilimia 50-70 na masomo yenye ufaulu wa chini
ni Chemistry, Basic Maths, Physics, Commerce na Agriculture ambayo
ufaulu wake ni chini ya asilimia 50.
Amesema katika baadhi ya masomo, baadhi ya wanafunzi wameonesha umahiri kwa kufaulu kwa kupata alama 100%.
Masomo hayo ni
Englishi wanafunzi 41
Basic Maths wanafunzi 9
Biology mwanafunzi 1 na Book keeping mwanafunzi mmoja.
Ameipongeza
serikali kwa kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kwa madai
kuwa ndiyo sababu ya matokeo haya kuwa mazuri lakini ametaka juhudi
ziendelee kufanywa katika masomo yenye ufaulu wa chini.
tiko
tiko
Post a Comment