tiko
tiko
POLISI wa mikoa ya Mwanza, Simiyu na Shinyanga wamefanikiwa kusambatarisha mtandao wa ujambazi kwenye mikoa hiyo baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa ujambazi sugu, Njile Samweli (46) mkazi wa kijiji cha Lyoma, Bariadi mkoani Simiyu aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu.
Sambamba
na kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo wa ujambazi, pia watuhumiwa watano
wanashikiliwa, bunduki moja yenye namba PB 3402 aina ya SMG na risasi
331 na kwamba operesheni ya kina inaendelea kwa lengo la kuwakamata
watuhumiwa wote pamoja na silaha wanazotumia.
Wakizungumza
kwa pamoja Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola alisema
Januari 5, mwaka huu majira ya saa 7 mchana walimkamata Mabula Lyagwa
(36) akiwa na jeraha la risasi kwenye bega lake la kulia baada ya
kupokea taarifa kutoka kwa raia wema.
Alisema
mtiliwa shaka huyo alipohojiwa alisema kuwa jeraha hilo alipigwa risasi
na jambazi mwenzake aitwaye Njile Samweli wakati wakifanya tukio la
ujambazi katika kijiji cha Idukilo kata ya Mwadui Luhumbo wilayani
Kishapu mkoani Shinyanga Januari 5, saa sita za usiku.
Alisema
kutokana na maelezo hayo kikosi cha upelelezi mkoani hapa kiliungana na
mikoa mingine na kufanya msako uliofanikiwa kumkamata Njile Samweli
ambapo alipohojiwa alikiri kuhusika na matukio mbalimbali ya unyang’anyi
wa kutumia silaha katika mikoa ya Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Tabora na
Singida.
Alisema
mkoani hapa, mtuhumiwa huyo pamoja na wenzake wamefanya matukio
mbalimbali ya uhalifu ambapo Agosti mwaka jana walivamia nyumba ya
kulala wageni kwenye kisiwa cha Bulubi, wilayani Ukerewe na kupora Sh
milioni 3.5 za wafanyabiashara wa dagaa.
Pia
tukio jingine walilifanya Oktoba 2, mwaka jana katika kijiji cha Mahaha
wilayani Magu ambapo walivamia maduka na kupora Sh milioni 3 pamoja na
pikipiki aina ya Sanlg na kumuua mtu mmoja na kwamba mwezi huo huo
walivamia Ngudu ambapo walimjeruhi kwa risasi mtu mmoja na kumpora Sh
milioni 2.
Naye
Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo alisema mtuhumiwa huyo
kwa kushirikiana na wenzake watano wakiwa na silaha SMG No. BP 3402
pamoja na magazine yenye risasi 40 na kiroba kimoja kikiwa na risasi
nyingi mali ya Mahenga Nkinda wakiwa ndani ya Hifadhi ya Mawa wakiwinda
tembo na faru, ilipofika saa sita usiku, Njile aliamka na kuchukua
silaha hiyo na kuwaua wenzake aliokuwa nao kisha kwenda kuichimbia
nyumbani kwake.
Alisema
Agosti 18, mwaka jana walifanya uvamizi katika duka la mfanyabiashara
Igunga na kuua mtu mmoja, kisha aliunda kikosi kingine cha ujambazi
ambacho mwezi huo huo walimuua mfanyabiashara wa ng’ombe na kufanikiwa
kupora Sh milioni 18 na matukio mengi mawili yaliyofanyika wilayani
Maswa ya kuvamia maduka ya wafanyabiashara na kupora.
Kwa
upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Justus Gamgisha
alisema Januari 5, mwaka huu Njile na kundi lake walifanya uvamizi
katika kijiji cha Idukilo ambapo walivamia maduka manne na kupora Sh
milioni 3.2 pamoja na simu aina ya Nokia baada ya kufyatua risasi hewani
ambapo moja ilimjeruhi jambazi mwenzao Mabula Lyagwa
tiko
tiko
Post a Comment