tiko
tiko

Manchester United imethibitisha kuwa itafanya jaribio la mwisho la kumsajili beki wa kimataifa wa Ujerumani Mats Hummels zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili la mwezi januari .
United imekuwa ikimsaka Mats Hummels tangu wakati wa dirisha kubwa la usajili la majira ya kiangazi ambapo beki huyo alisisitiza kuwa angependa kuendelea kubaki na timu yake Borrusia Dortmund lakini United bado haijakata tamaa ya kumsajili .
Beki wa Borrusia Mats Hummels amekuwa akisakwa kwa udi na uvumba na Manchester United.

Beki
wa Borrusia Dortmund Mats Hummels amewekwa kama mchezaji namba moja
kwenye orodha ya wachezaji ambao Manchester United inataka kuwasajili .
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ambavyo viko ndani ya United klabu hii itajaribu kusajili mmoja kati ya wachezaji hawa ili kuimarisha safu yake ya ulinzi huku wakiwa kwenye vita ya kuwania nafasi ya kufuzu michunao ya ligi ya mabingwa .

Beki Mfaransa Aymeric Laporte amewekwa kwenye orodha ya usajili ya Manchester United kama mbadala wa Mats Hummels .
tiko
tiko
Post a Comment