Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

Mtazame Mke wa Star wa Real Madrid akiwa uwanjani .

tiko tiko
james no 10

Siku zote waarabu wa Pemba hufahamiana kwa vilemba na ndege wa mabawa ya kufana hupaa pamoja , msemo huu unaonekana kuwa kweli kwa familia ya nyota wa Real Madrid na timu ya taifa ya Colombia James Rodriguez ambaye hivi karibuni alionekana akiwa kwenye uwanja wa mchezo wa Volleyball  akiwa anamtazama mke wake .
Mke wa James Rodriguez ambaye anaitwa Daniella Ospinna ni mchezaji wa timu ya Real Madrid ya mchezo wa  Volleyball na James siku za hivi karibuni ameonekana akiwa kwenye uwanja kumtazama mkewe .
Daniella kama ilivyo kwa mumewe anavaa jezi nambari 10katika timu hiyo ya Real Madrid na ameonekana kuwa mchezaji muhimu sana hasa kutokana na urefu wake ambao ni kitu muhimu kwa mchezo wa Volleyball hasa kwa mchezaji wa kati .
James Rodriguez akiwa anamtazama mkewe akiwa uwanjani huku akiwa amembeba  mtoto wao .
James Rodriguez akiwa anamtazama mkewe akiwa uwanjani huku akiwa amembeba mtoto wao .
Rodriguez ambaye alisajiliwa na Real Madrid akitokea As Monaco baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya kombe la dunia amezidi kufanya vizuri akiwa na timu yake mpya ambayo hadi sasa ameifungia mabao 10 kwenye mechi 30 ambazo amecheza kwenye michuano mbalimbali na siku hadi siku umuhimu wake unazidi kuongezeka .
Daniella Ospina akiwa uwanjani anakoiwakilisha klabu ya Real Madrid ya mchezo wa Beach Voleyball.
Daniella Ospina akiwa uwanjani anakoiwakilisha klabu ya Real Madrid ya mchezo wa  Voleyball.    
Daniella Ospinna anatokeo kwenye familia ya michezo ambapo ana undugu wa damu na kipa namba moja wa Colombia maybe pia huichezea Arsenal David Ospinna na kipa huyo ndio hasa alimkutanisha dada yake na James Rodriguez ambaye ni rafiki yake wa muda mrefu na urafiki huo sasa umekuwa undugu ambapo wawili hao sasa wanaitana shemeji .

daniela ospina

danielaaa

rodriguezzz
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top