tiko
tiko

Wagombea wawili wa nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa FIFA Luis Figo na Prince Ali Bin Al Hussein wametangaza kupita hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye uchaguzi huo .
Haua hiyo inahusisha kuteuliwa kwa kutiliwa saini na vyama vitano vya soka toka kwenye nchi wanachama wa fifa .
Mchezaji wa zamani wa Ureno na klabu za Sporting Lisbon , Fc Barcelona , Real Madrid na Inter Milan Luis Figo na Rais wa chama cha soka cha Jordan ambaye pia ni makamu wa rais wa Fifa Prince Ali Bin Al Hussein ni moja kati ya watu sita ambao hadi sasa wametangaza dhamira ya wazi ya kuingia kwenye mbio hizo za kuwania urais wa Fifa .

Luis
Figo amekidhi moja ya vigezo muhimu vya kugombea urais wa Fifa baada ya
kuidhinishwa na vyama vitano vya soka toka barani ulaya .
Inaaminika kua vyama vya soka vya Denmark , Ureno , Montenegro , Macedonia , Luxembourg na Poland ndio vyama vilivyompitisha Figo .
Kwa upande wake Prince Ali alithibitisha kupitia kwenye kigezo hicho ambapo alitumia ukurasa wake binafasi wa Twitter kuwaeleza watu wake kuwa tayari amepata saini za vyama vitano .
Hadi sasa Ukiachilia mbali Figo na Pirnce Ali wagombea wengine waliojitokeza ni mchezaji wa zamani wa Ufaransa David Ginola , Kiongozi wa zamani wa Fifa Jerome Champagne , rais wa chama cha soka cha UHolanzia Michel Van Praag pamoja na rais wa sasa Sepp Blatter
tiko
tiko
Post a Comment