tiko
tiko
Mwanamke
aliyetambulika kwa jina la Hawa Kundani amezua taharuki kwenye kikao
cha Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, baada ya kuvamia
ghafla na kupiga kelele akidai kutelekezwa na mumewe ambaye ni Mbunge wa
Dimani (CCM) visiwani Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir.
Tukio
hilo la aina yake lilitokea jana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa
wa Mwalimu Nyerere, na mwanamke huyo akiwa ameongozana na mtangazaji wa
kituo kimoja cha redio, Joyce Kiria aliingia na kusababisha mshtuko kwa
wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wa dini ya Kikristo waliokuwa
wamealikwa hapo. Wakati huo walikuwa wakijadiliana suala la Mahakama ya
Kadhi.
Hawa
akizungumza na paparazi alidai kwamba Ameir ni mume wake walifunga ndoa
mkoani Arusha mwaka 1999 na kuzaa naye watoto wanne, lakini mmoja
alifariki dunia.
“
Nashangaa amebadilika ghafla amekuwa mtu wa kuoa wanawake na kuacha
mara kwa mara, hadi sasa ameshaoa wanawake wanne na kuwaacha mimi nipo
tu, alinioa bado mdogo,” alidai Hawa.
Alidai
kuwa watoto wengine wawili, mkubwa ana miaka tisa na mwingine miaka
sita walichukuliwa na mumewe huyo akawapeleka kulelewa na mwanamke
aliyemuoa jambo ambalo alidai linamuuma.
“
Naumia wanangu sijui wanaishi vipi, huyu niliyembeba ni mlemavu,
hamtaki amekuwa akininanga kwa maneno mengi sana, mimi nimetoka naye
mbali nilibadili dini kwa ajili yake, leo hii ananitesa, hanitaki anipe
haki yangu ili niishi mwenyewe,” alisema Hawa.
Kwa
upande wa mbunge hiyo Ameir alidai kwamba kesi yao ipo kwenye Mahakama
ya Kadhi, akidai kwamba mwanamke huyo amekuwa akimdhalilisha kwa kupitia
mtoto huyo mlemavu ambaye alikiri ni mwanaye.
“
Huyu ni mwanangu sishindwi kumhudumia, lakini sitaki fedha ziende kwa
huyu mwanamke atazitumia kwa mambo yake mengine, mimi nilimpeleka kwa
mama yake mzazi akakae naye huko lakini yeye hataki,” alisema Mbunge
Ameir.
Akizungumzia
tukio hilo Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Gosbert Blandes alisema ni
tukio ambalo limewafedhehesha kwa kuwa hawakulitarajia.
“Tulivamiwa
na wanawake kama wanne na wanaume wawili nafikiri mmoja alikuwa ni
mpiga picha, mwanamke mmoja akawa anapiga kelele, tulitaharuki kwa
sababu maaskofu walikuwa wameanza kutoa maoni yao,” alisema.
Alisema
kwamba waliomba msaada kwa maofisa usalama wa ukumbi na walifika na
kuwachukua wahusika hao, kisha kuwapeleka polisi kwa hatua zaidi.
tiko
tiko
Post a Comment