tiko
tiko
KAMBI rasmi ya upinzani bungeni imesema itawasaidia kwenye masuala ya kisheria wanafunzi waliofukuzwa kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kutokana na kuandamana kudai kupewa fedha za kujikimu.
Akizungumza
juzi katika ofisi za Bunge, Waziri Kivuli wa Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi, Susan Lyimo alisema kuwa tatizo hilo linatokana na serikali
kutokuwa na mipango ya kuhakikisha maslahi ya wanafunzi hao
yanatekelezwa.
Alisema
watawasaidia masuala ya kisheria kuhakikisha wanarejeshwa chuoni kwani
walichokifanya ni haki na kusema hawezekani wanafunzi wakakaa chuoni kwa
miezi mitatu bila kupewa fedha za kujikimu.
Juzi
uongozi wa chuo hicho uliwaachisha masomo wanafunzi watatu vinara wa
maandamano hayo ya wanafunzi wa programu maalum ya walimu wa sayansi.
Mmoja
wao alifukuzwa moja kwa moja na wawili wana nafasi ya kujieleza
kuhusika kwao na maandamano hayo yaliyochafua hali ya hewa na
kusababisha wanafunzi 84 kutiwa mbaroni.
Walioondolewa
shuleni ni Kyambwene Msatu(Rais wa serikali ya wanafunzi), Philip
Mwakibinga (Waziri Mkuu) na Ismail Chande (Katibu Mkuu).
tiko
tiko
Post a Comment