tiko
tiko
Mwanadada asiyeishiwa habari, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
MWANADADA asiyeishiwa habari, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ anadaiwa kujutia mimba yake aliyopachikwa na aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ wakati wa mapenzi yao.
Chanzo makini kilicho karibu na Wema
kilieleza kwamba, mwanadada huyo kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu huku
akijutia mimba aliyopewa na Kanumba ambayo ilichoropoka kwa bahati mbaya
na huyo ndiye mwanaume pekee aliyewahi kumpa ujauzito.
“Yaani Wema anajutia kweli kwamba kwa
nini hakuzaa na Kanumba kwani ndiye mwanaume pekee aliyewahi kumpa
ujauzito ambapo kwa sasa anatafuta mtoto lakini hapati, yaani yupo
kwenye wakati mgumu sana akikuelezea mwenyewe unaweza kulia kwani ana
simulizi ya kusikitisha kuhusu maisha yake na Kanumba.
“Hii yote inatokana na kwamba kwa sasa anatamani kuitwa mama lakini hapati hivyo kujikuta akiukumbuka ule ujauzito wa Kanumba anateseka kweli moyoni,” kilisema chanzo hicho.
“Hii yote inatokana na kwamba kwa sasa anatamani kuitwa mama lakini hapati hivyo kujikuta akiukumbuka ule ujauzito wa Kanumba anateseka kweli moyoni,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa Wema kuhusu ishu hiyo alikiri na kuonesha namna gani anateseka moyoni.
“Nateseka kweli, tangu ilipotokea kwa Kanumba haijawahi kutokea tena. Hakuna mtu ambaye hapendi kuwa mama, nazidi kumuomba Mungu huenda na mimi itatokea nitapata,” alisema Wema.
“Nateseka kweli, tangu ilipotokea kwa Kanumba haijawahi kutokea tena. Hakuna mtu ambaye hapendi kuwa mama, nazidi kumuomba Mungu huenda na mimi itatokea nitapata,” alisema Wema.
tiko
tiko
Post a Comment