tiko
tiko
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
Wakati
makundi mbalimbali yakipigana vikumbo kumshawishi aliyekuwa Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo agombee urais, mwenyewe
amesema muda bado, ukifika atasema.
Baadhi
ya makundi yaliyojitokeza na kumtaka agombee ni Chama cha Watu wenye
ulemavu mkoani Mwanza na wanafunzi wa vyuo vikuu vya Jomo Kenyatta, IAA,
Semmco na Makumira.
Akiwa
bungeni mjini Dodoma, Profesa Muhongo amekuwa akitajwa mara kwa mara na
wabunge wenzake kama rais mtarajiwa na yeye amekuwa akifurahia kuitwa
hivyo.
Lakini tulipomuuliza kuhusu suala hilo, alijibu “Ya kwangu nitayasema muda ukifika.”
Alisema
kama kuna watu wanamuunga mkono hawezi kuwazuia, ila wasiandamane
kumfuata kwa nia ya kumshawishi kwani kufanya hivyo ni kinyume na
taratibu.
Machi
22 mwaka huu, kupitia mwenyekiti wao, Charles Ngereza wanafunzi hao
waliwaambia waandishi wa habari jijini Arusha kuwa watazunguka kwenye
vyuo na taasisi zote za elimu ya juu nchini kuwashawishi wenzao kuungana
nao.
“Sababu
kuu ya kumuunga mkono ni rekodi ya utendaji wake. Kwa kipindi kifupi
alichoongoza Wizara ya Nishati na Madini amefanya mapinduzi makubwa
yaliyowashinda watangulizi wake ikiwamo kushusha bei ya kuunganisha
umeme kufikia kati ya Sh27,000 hadi Sh177,000 vijijini,” alisema
Ngereza.
Alisema
kasi ya utekelezaji wa mradi wa umeme vijijini, licha ya kuwapatia
wananchi huduma ya nishati, pia imechangamsha uchumi kwa kuongeza
shughuli za uzalishaji zinazotegemea nishati ya umeme.
Muhongo: Ni mapema mno
Profesa Muhongo alisema kuwa ni mapema sana kuzungumza kama atawania urais au la.
“Hawajaja (wanafunzi) kuniona kama wanataka (kunishawishi) waendelee huko huko si kuja kwangu,” alisema.
Aliongeza, “Taratibu zimewekwa mbona mnakuwa na wasiwasi, ya kwangu nataka nikiyaongea muda uwe umefika.”
Katika
hoja zao wanafunzi hao, walisema hatua ya Profesa Muhongo kujiuzulu
ilitokana na uwajibikaji kutokana na dhamana aliyokuwa nayo.
Walisema
hiyo ni moja ya sifa za uongozi na kumtaja Rais mstaafu wa awamu ya
pili, Ali Hassan Mwinyi aliyejiuzulu uwaziri wakati wa uongozi wa
Mwalimu Julius Nyerere na baadaye kuukwaa urais.
Wanafunzi
waliohudhuria mkutano huo na vyuo vyao kwenye mabano ni Rahma Sengela
(Jomo Kenyatta), Daudi Shayo (IAA), Sarah Aminarabi (Arusha), Nelson
Machumu (Semmco) na Hobeshi Juvenary kutoka Makumira.
tiko
tiko
Post a Comment