tiko
tiko
WATU sita wamekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 40.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja
Juma Saad Khamis, alisema hilo ni moja ya matukio mabaya kuripotiwa
kufanywa katika kipindi cha maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka.
“Watu hao walikamatwa Jumapili saa 2 usiku wakihusishwa kuhusika na tukio hilo,” alisema.
Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa siku
ya tukio watuhumiwa walionekana wakinywa na mwanamke huyo na baadaye
walianza kumpiga na kumchukua hadi maeneo ya Bwejuu.
Hata hivyo Kamanda Khamis alikataa kutoa
maelezo ya kina kuhusiana na watuhumiwa hao kwa maelezo kuwa yanaweza
kuvuruga upelelezi wa tukio hilo ambao unaendelea kufanywa na mamlaka
husika.
Alisema ukiacha tukio hilo baya, wananchi walisherehekea kwa amani sikukuu ya Pasaka.
“Kulikuwa na amani, nawashukuru polisi
wa doria kwa kazi yao nzuri na kusababisha wananchi kusherehekea sikukuu
kwa amani,” alisema Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Mkadam Khamis
Mkadam.
Kamishna Msaidizi (ACP) Mkadam alisema
kulikuwa na matukio madogo ya ajali za barabarani, naye Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mohamed Msangi alisema katika mkoa
wake hakukuwa na matukio mabaya
tiko
tiko
Post a Comment