tiko
tiko
Mahakama
Kuu ya Tanzania, leo imetupilia mbali shauri lililofunguliwa na Zitto
Zubeir Kabwe mwaka jana, akipinga kikao cha Kamati Kuu ya Chadema
kumjadili, akikitaka chombo hicho cha sheria, kukielekeza chama chake,
kusubiri kwanza rufaa yake aliyokuwa amekata katika Baraza Kuu.
Mahakama
iliyoketi chini ya Jaji Mziray, ilikubaliana na hoja za mawakili wa
Chadema, waliosema kuwa ufunguaji wa kesi hiyo ulikiuka baadhi ya
vifungu vya sheria na hivyo kumtaka mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini
kulipa gharama zote za kesi hiyo.
Baada
ya hukumu hiyo, Zitto Kabwe amesema hakuwa na wito wa mahakamani
leo na Jaji aliyekuwa akiisikiliza kesi hiyo amehamishiwa Tabora,
hivyo mwanasheria wake ameenda kufuatilia mazingira ya hukumu
hio.
"Hatuna taarifa ya Jaji Mpya. Mwanasheria wetu anafuatilia na atatoa statement", ameandika Zitto Kabwe katika ukurasa wake wa twitter.
Wakati Zitto akifungua kesi hiyo Januari mwaka jana, tayari Chadema ilikuwa imewafukuza uanachama Dr. Kitilya Mkumbo na Samson Mwigamba ambao pamoja na Zitto, walituhumiwa kupanga njama za kufanya mapinduzi ya uongozi ndani ya chama hicho.
Zitto alikuwa akitetewa na wakili Albert Msando wakati Chadema iliwakilishwa na Tundu Lissu, Peter Kibatala na John Mallya.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko




Post a Comment