tiko
tiko
Barabara ya Shekilango maeneo ya Sinza ilivyo na sehemu zilizowekewa zege kwenye mitaro ili kupitisha magari na wateja.
WAFANYABIASHA katika maduka barabara ya Shekilango, jijini Dar es
Salaam, wanasemekana kukwamisha mifereji ya uchafu kwa kujenga njia za
zege ili kuwezesha kupitisha kwa urahisi magari yao na wateja.
Mifereji hiyo hushindwa kufanya kazi kutokana na taka ambazo hunaswa
chini ya ‘vivuko’ hivyo.
Tukio hilo limethibitishwa na kamera yetu ambapo kitendo hicho
kinaonekana kukwamisha mapito ya maji kwa urahisi, na hivyo kujaa sehemu
za barabarani.
Mtandao huu ulihojiana na wapita njia sehemu hiyo ambao walikuwa na
maoni kwamba mifereji hiyo inachangaia kuziba mifereji ya maji machafu
wakati wa mvua.
Mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta msemaji wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS) ili kuzungumzia suala hilo ambapo simu yake
iliita bila mafanikio na alipotumiwa ujumbe wa maneno hakuweza kujibiwa.
tiko
tiko
Post a Comment