tiko
tiko
KANISA la Presbyterian nchini Marekani
ambalo lina wanachama milioni mbili, limebadilisha sheria yake ya ndoa
na kuwajumuisha watu wa jinsia moja.
Kanisa
hilo ambalo linashirikisha idadi kubwa ya wanachama wake duniani
lilitoa tangazo hilo baada ya idadi kubwa ya magavana wa majimbo yake
171 kuidhinisha mabadiliko hayo.
Sheria yake mpya sasa itasoma kwamba
ndoa ni makubaliano ya kipekee kati ya watu wawili ikilinganishwa na
makubaliano kati ya mume na mke.
Sheria hiyo iliyoidhinishwa na baraza kuu la kanisa hilo mwaka uliopita ilikubaliwa na zaidi ya nusu ya majimbo ya kanisa hilo.
Uamuzi huo unatarajiwa kuzua mgawanyiko mkubwa kati ya wanachama wa kanisa hilo ambao wanapinga sheria hiyo.
tiko
tiko
Filed Under:
BURUDANI
Post a Comment