tiko
tiko
VIDEO inayomuonyesha
msichana anayefanana kwa sura na umbo na staa wa filamu, Amanda Poshi,
imemfanya msanii huyo ajikute katika mateso makubwa kisaikolojia, kwani
wengi wanaamini ni yeye.
Staa wa filamu za kibongo, Amanda Poshi.
Akizungumza na gazeti hili, Amanda alisema ameumizwa sana na video hiyo
ambapo mwanamke huyo anakata mauno ya haja kwani imesambaa sehemu
mbalimbali kiasi cha baadhi ya watu kuwapigia simu wazazi wake
wakimlalamikia.
“Jamani mimi siyo huyo mwanamke anayekata mauno na simfahamu, kwanza
hata ukiangalia vizuri yeye ni mweusi na siyo mnene kama mimi hivyo
nawaomba mashabiki wangu wajue kwamba siwezi kujidhalilisha kiasi
hicho,” alisema Amanda.
tiko
tiko
Post a Comment