tiko
tiko
CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT) kinategemea kuanzisha benki yake
itakayojulikana kama Mwalimu Commercial Bank baada ya maombi ya kuuza
hisa za benki hiyo kukubaliwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana
(CMSA) kwa ajili ya kuanza kuuza hisa hizo. Hisa hizo zinatarajiwa
kuanza kuuzwa kwa walimu na Watanzania wote kuanzia Machi 23 hadi Mei 4
mwaka huu.
Hayo yalisemwa leo na Rais wa CWT, Gratian Mukoba, kwa wanahabari na
kufichua kwamba benki hiyo inatarajiwa kufungua milango yake Novemba 2
mwaka huu ambapo anategemea itaanza kwa mtaji usiozidi sh. Bilioni 25.
Chama hicho kimeweka kivutio cha 50,000/= kutoka kwa kila mwalimu,
kiwango ambacho kitamwezesha kununua hisa 100 katika benki yake hiyo.
‘’Ninaomba ieleweke kuwa kama nilivyokwishaeleza hapo awali kuwa
tunategemea kuanza kuuza hisa zetu tarehe 23 Machi 2015 na uuzwaji wa
hisa hizi utaweza kuchukua kipindi cha wiki sita, baada ya hapo
tutapeleka majina ya wanahisa wetu Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa ajili
ya uhakiki na benki yetu kupatiwa leseni yake tayari kwa kuanza
biashara, hivyo hisa zitaorodheshwa kwenye soko la hisa tarehe 8 Juni,
2015,’’ alisema Mukoba.
Kiongozi huyo wa CWT aliongeza kwamba kutokana na idadi ya walimu ambao
ni zaidi ya laki mbili nchini, pamoja na Watanzania wengine, watapata
wananchama wapatao laki tatu, hivyo aliwaomba wananchi wajitayarishe kwa
ununuzi wa hisa hizo.
tiko
tiko
Post a Comment