tiko
tiko
Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mch. Chrostopher Mtikila
MCHUNGAJI
Christopher Mtikila, leo amefungua kesi ya kikatiba namba 14 ya mwaka
2015 katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga muswada wa mabadiliko ya
sheria kwa ajili ya kuitambua rasmi Mahakama ya Kadhi. Deusdedit Kahangwa anaripoti…(endelea).
Muswada
huo umepangwa kuwasilishwa, kujadiliwa na kupitishwa katika kikao cha
Bunge litakaloanza vikao vyake Jumanne wiki hii mjini Dodoma.
Katika
mashtaka yake, Mchungaji Mtikila aliye Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha
Democratic (DP), anaitaka mahakama kuu kufanya mambo makuu matatu.
Kwanza, anaitaka imwadhibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, kwa kumpa kifungo kisichopungua miaka mitano kutokana na kitendo chake cha jaribio la kuvunja ibara ya 19 ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.
Pili,
anaitaka itamke kwamba ni kinyume cha sheria kwa serikali kujihusisha
katika masuala yoyote yanayohusu Mahakama ya Kadhi au Shirika la
Waislamu Duniani (OIC).
Na
tatu, anaitaka Mahakama Kuu itamke kwamba adhabu zinazotolewa na
Mahakama ya Kadhi kwa mujibu wa sheria za Kiislam (sharia), kama vile
viboko, kupondwa mawe hadi kufa, kukata kichwa, na kukata mikono,
zinapingana na utu wa binadamu, na ni kinyume cha Tamko la Umoja wa
Mataifa Kuhusu Haki za Binadamu.
Kwa
mujibu wa hati ya mashtaka iliyo mikononi mwa MwanaHALISIOnline,
mshitakiwa mkuu ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, ambaye
ni mshauri mkuu wa serikali kuhusu masuala yote ya kisheria. Masaju
anakabiliwa na mashtaka makuu mawili.
Kwanza,
Mtikila anamtuhumu Masaju kushirikiana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
mawaziri Mary Nagu, Asha-Rose Migiro na mawakala mbalimbali katika
kuratibu uanzishwaji wa “Mahakama ya Kadhi” kazi ambayo ni sehemu ya
mradi mpana wa “kuibadilisha Tanzania kuwa dola ya Kiislam.”
Kwa
mujibu wa Mtikila hili ni jaribio la “kuipindua serikali ya
kidemokrasia na isiyofungamana na dini yoyote katika Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania,” na badala yake kusimika mfumo wa serikali yenye mnasaba
na dini ya Kiislam “chini ya usimamizi wa makadhi.”
Mtikila
anadai kwamba, kwa mujibu wa sheria za Kiislam (sharia), kiongozi
aitwaye “Kadhi Mkuu” anapaswa kuwa na mamlaka ya pili baada ya rais wa
nchi.
Hivyo,
anasisitiza kuwa mfumo huu wa kisheria utawainua waislamu wapatao
milioni 12.4 dhidi ya Wakristo wapatao milioni 29 hapa nchini Tanzania.
“Muswada
kuhusu Mahakama ya Kadhi haukubaliki Tanzania kwa kuwa ni wa kibaguzi,
kwani unawahusu Wasislam pekee ambao ni sehemu ndogo ya wananchi, na
hivyo utawafanya wananchi baki kuwa watumwa wa waislam, jambo ambalo ni
kinyume cha ibara za 12, 13(2), 13(4), 13(5) na 19 katika Katiba ya
Tanzania ya mwaka 1977,” anasema Mtikila.
Kwa
mujibu wa Mtikila Wakristo hao milioni 29 wanajumuisha Walutheri
milioni 5.5, Wakatoliki milioni 11, Waanglikana milioni 3, Wamoraviani
milioni 1.8, Wapentekoste milioni 5.8, Waadventisti milioni 1.8 na
waumini wa dini za asili milioni 7.
Pili,
Mtikila anamtuhumu Masaju kushirikiana na Waziri Stephen Wasira,
Mizengo Pinda, Ernest Ndikilo, Karen Yunus, Issa Njiku, Dan Makanga, na
Ernest Mangu kusigina katiba ya nchi kwa kuwaweka Wakristo milioni 29
chini ya utumwa wa Kiislam, kwa kuwazuia kuchinja mifugo yao kwa ajili
ya kitoweo, na badala yake kuwataka wale kitoweo kutokana na wanyama
waliochinjwa na Waislam.
Kwa
mujibu wa mchungaji Mtikila, jambo hili ni kinyume cha Sheria ya
Magonjwa ya Wanyama ya mwaka 2003; kinyume cha Sheria ya Chakula, Madawa
na Vipodozi ya mwaka 2003; na kinyume cha ibara ya 19 ya Katiba ya
Tanzania ya mwaka 1977.
Kwa
kuzingatia tuhuma hizi, Mtikila anaiomba Mahakama Kuu kumtaka
Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na washirika wake kujieleza ni kwa
nini wasifungwe jela kwa miaka mitano na zaidi kwa kosa la kuisigina
katiba ya nchi ambayo walikula kiapo cha kulinda na kuitetea.
Mtikila
amefungua mashtaka hayo kwa kutumia mamlaka yake kama raia wa Tanzania
mwenye jukumu la kuilinda katiba ya nchi dhidi ya dharau na usiginaji
mwingine wa aina yoyote. Mamlaka hayo anapewa na ibara ya 26(2) ya
Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.
tiko
tiko
Post a Comment