Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

Viongozi Watatu wa CHADEMA Wanaotuhumiwa Kumteka na Kumtesa Mlinzi wa Dr. Slaa Wapata Dhamana.

tiko tiko

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imewaachia kwa dhamana viongozi  watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwamo Diwani wa Kata ya Ubungo, Boniface Jacob (32) wanaokabiliwa na mashtaka mawili ya kuteka na kujeruhi.

Mbali na Jacob, washitakiwa wengine ni Mkuu wa Walinzi, Hemed Sabula (48) na Ofisa Utawala wa chama hicho, Benson Mramba (30).

Wote waliachiwa baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Walifikishwa mahakamani wakituhumiwa kumteka aliyekuwa mlinzi wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, Khalid Kagenzi.

Jana saa 3:00 asubuhi washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza dhamana.

 Washtakiwa hao walisomewa mashtaka dhidi yao wiki iliyopita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanadaiwa kuwa Machi 7, mwaka huu, walimjeruhi na kumteka nyara Kagenzi kwa nia ya kuzuia uhuru wake.

Wakili wa Serikali, Janeth Kitale, alidai washtakiwa hao walifanya makosa hayo kinyume cha kifungu cha 225 na 249 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Pia alidai kuwa Machi 7, mwaka huu, washitakiwa hao kwa pamoja wakiwa katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo Mtaa wa Ufipa, Kinondoni, walimjeruhi Kangezi maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Wakili huyo aliendelea kudai kuwa siku hiyo ya tukio washtakiwa hao kwa pamoja, wakiwa katika ofisi hizo za Chadema, walimteka Kagenzi na kumpeleka Hoteli ya River View, iliyopo Sinza.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa wote walikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top