tiko
tiko
Hata hivyo kiasi kinachohitajika ni Sh78
bn ili kujenga barabara za juu kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) hadi katikati ya mji.
Hayo yamesemwa leo la Waziri wa Ujenzi,
Dk John Magufuli mjini Dodoma alipokuwa alipokuwa akijibu swali la
nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Rita Mlaki (CCM).
Dk. Magufuli alisema Serikali ina nia
ya dhati ya kupunguza msongamano wa magari kwa Jiji la Dar es Salaam
ndio maana inajenga Fly Over katika barabara mbalimbali za jiji hilo.
Katika swali la msingi la msingi, Mbunge
wa Viti Maalum, Mariam Kisangi (CCM), alitaka kujua mpango wa serikali
wa kuendeleza mji wa Kigamboni.
Pia alihoji mpango wa serikali wa kujenga kiwanja cha ndege katika mji huo wa Kigamboni.
Akijibu, Naibu Waziri wa Uchukuzi,
Chalres Tizeba, alisema serikali inayo mipango ya kuendeleza Mji wa
Kigamboni chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Uendeshaji wa Mji wa huo.
Tizeba alisema mji huo umo ndani ya Jiji la Dar es Salaam ambako JNIA
kipo.
“Kiwanja hiki kina uwezo wa kuhudumia
ndege zipatazo 30 kwa saa baada ya kukamilika kwa upanuzi wa miundombinu
na ukarabati wa awamu ya pili uliofanyika kati ya mwaka 2008 na 2011,”
alisema.
Alisema kwa sasa kiwanja kinahudumia wastani wa ndege nane kwa saa ambazo ni chini ya wastani.
Alisema mpango uliopo ni wa kupanua JNIA kwa kujenga jengo jipya la tatu la abiria.
tiko
tiko
Post a Comment