tiko
tiko
Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli
akikagua ujenzi wa kituo cha Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (BRT)
Morocco jijini Dar es Salaam siku za hivi karibuni. Picha na Maktaba
Machungu
ya Watanzania yakiwa hayajapoa kutokana na kashfa ya Sh306 bilioni
kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow, ufisadi mwingine wa zaidi ya
Sh252 bilioni umeibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad ndani ya wizara ya ujenzi.
Ukaguzi maalumu uliofanywa na ofisi ya
CAG katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/11 na 2011/12 umebaini kuwa
taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, bungeni
Novemba 2013 kuwa fedha hizo zilitumika kwa miradi ya ujenzi wa
barabara, haikuwa sahihi.
Kutokana na ufisadi huo, habari
zilizolifikia Mwananchi zinasema CAG amependekeza hatua stahiki
zichukuliwe kwa wahusika wa wizara ya ujenzi na wakala wa barabara ili
kuleta imani na uwazi katika bajeti kwa jamii na wahisani.
“Wizara (ya ujenzi) ililidanganya Bunge
kuwa kuna ujenzi wa barabara hizo wakati wakijua kwamba walikusudia
kulipa madeni ya wakandarasi na washauri wa ujenzi wa barabara...mpango
mkakati wa wakala wa barabara wa mwaka wa fedha 2011/12 pamoja na
manunuzi ulioidhinishwa havikuonyesha utekelezaji wa mradi huo,” chanzo
cha habari kilikariri ripoti ya CAG.
Matumizi hayo yasiyo sahihi yaliibuliwa
na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) Novemba 22, 2013 baada ya kutilia
shaka kiasi hicho cha fedha na ofisi ya CAG kuagizwa kufanya ukaguzi.
Katika kikao hicho ambacho wizara ya
ujenzi iliwakilishwa na Katibu Mkuu wake wa wakati huo, Balozi Herbert
Mrango alihojiwa na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe kuhusu hati ya
mashaka waliyoipata kutoka kwa CAG mwaka 2011/12.
Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti
ya mwaka huo Sh348.1 bilioni zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu
lililokuwa limetajwa kuwa ni la mradi maalumu hazikutumiwa kwa malengo
yaliyoelezwa bungeni.
“Ni vizuri leo (ilikuwa Novemba 22 mwaka
2013) uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika
kwa jambo gani. Tunajua kwamba fedha hizi zilipunguzwa Sh95 bilioni na
kupelekwa Wizara ya Uchukuzi, zilibakia Sh252.975 bilioni katika kifungu
hicho lakini kuna bilioni 100 zimetumika visivyo,” alisema Zitto.
Alisema katika majumuisho ya bajeti
wizara hiyo, Dk Magufuli na Dk Harrison Makyembe aliyekuwa Naibu waziri
wa wakati huo aliyekuwa Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi
walitoa maelezo yasiyo ya kweli bungeni kuhusu fedha hizo.
Zitto alikariri maneno yaliyorekodiwa kwenye Hansard ya Bunge yaliyosemwa na viongozi hao watatu.
“Tunaomba fedha Sh252 bilioni kwa ajili ya kuanzia kazi za ujenzi wa barabara.”
“Fedha hizi zitachangia miradi ya
wafadhili,” haya yalikuwa maneno ya Dk Makyembe ambaye sasa ni Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati akifafanua majumuisho.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment