tiko
tiko
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu
za Serikali, Zitto Kabwe akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati
hiyo na wadau wa Sekta ya Utalii na Usafiri Dar es Salaam jana. Kulia ni
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahmoud Mgimwa. Picha na Said
Khamis
Kamati
ya Hesabu za Serikali (PAC), imetoa siku 113 kwa Msajili wa Hazina
(TR), Lawrence Mafuru kukamilisha mpango mkakati wa kuanzisha upya
Shirika la Ndege Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka za Hifadhi za
Ngorongoro na Tanapa.
Kauli hiyo ilitolewa kwenye ofisi ndogo
za Bunge Dar es Salaam wakati wa kikao cha mashauriano baina ya TR,
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Kamati hiyo
kilichofanyika jana na kukubaliana kuwa TR asimamie mchakato huo.
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alisema:
“Baada ya majadiliano kamati inamuagiza TR asimamie mchakato huu ambao
umekwisha anza miaka miwili iliyopita kuhakikisha ifikapo Juni 30, iwe
imewasilisha ripoti yake kabla ya Bajeti ya Serikali kuleta mpango
mkakati huo.”
Zitto aliongeza kuwa, “Tunataka kuwa na
shirika jipya linaloweza kujiongoza na TR ndiye ana wajibu wa hilo,
mchakato huu ulipoanza haukuwa umesimamiwa vizuri kwani hata TR mwenyewe
hakuwa anaufahamu lakini sasa tunamkabidhi jukumu hilo yeye mwenyewe.”
Alisema mapato wanayopata Tanapa na Ngorongoro yanaweza kununua ndege na wala si kuchangia mapato kama ilivyokuwa awali.
Kwa upande wake, Mafuru alisema: “Mimi
nitakwenda kutumia taarifa za kamati ambazo zilikwisha undwa na
kuangalia jinsi gani shirika litafufuliwa pamoja na maoni ya kamati
kisha nitakuja na kile ambacho kamati imekipendekeza.”
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL), Salim Msoma alisema, suala la wawekezaji hususani wa
nje halitakiwi kutegemewa kwani linapokuja katika utekelezaji wake,
miradi yake inakuwa na changamoto nyingi.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment