tiko
tiko
MAHAKAMA moja nchini Ivory Coast leo imemhukumu Simone Gbagbo aliyekuwa
mke wa Rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, kifungo cha miaka 20 gerezani.
Simone amehukumiwa kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki
katika vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi nchini humo mwaka 2010 -
2011 ambapo watu takribani 3,000 wlipoteza maisha.
Simone Gbagbo mwenye umri wa miaka 65 alikamatwa Aprili 11, 2011 pamoja
na mumewe, aliyekuwa rais wa nchi hiyo ambaye anakabiliwa na mashtaka ya
uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama ya uhalifu mjini The Hague,
Uholanzi.
Machafuko hayo yalitokea nchini Ivory Coast mwaka 2010 baada ya Laurent
Gbagbo kukataa kuachia madaraka kwa mpinzani wake Alassane Ouattara
aliyekuwa ametangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa rais.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment