tiko
tiko
Hashim Aziz
Miaka mitano aliyopewa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Mheshimiwa John Mnyika kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inaelekea kuisha lakini bado zipo changamoto mbalimbali ambazo zitamfanya mbunge huyo akitaka kurudi tena madarakani, afanye kazi ya ziada.

Miongoni mwa matatizo makubwa
yanayowasumbua watu wa Ubungo, ambayo licha ya Mnyika kujitahidi
kutafuta ufumbuzi mpaka leo hajafanikiwa kulitatua, ni tatizo la ukosefu
wa maji safi na salama.
Uwazi Mizengwe ya Uchaguzi, limefanya
mahojiano na wananchi kadhaa wa jimbo hilo lililopo jijini Dar es Salaam
ambapo wengi wamelalamikia kuwa suala la ukosefu wa maji ni kero namba
moja.
Ukiachilia mbali ukosefu wa maji safi na
salama, matatizo mengine yanayowasumbua wananchi ni ukosefu wa huduma
bora za kijamii zikiwemo hospitali, ukosefu wa ajira kwa vijana wengi
unaosababisha kuongezeka kwa matukio ya uhalifu hasa kwa wasafiri
watokao mikoani katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo.
Matatizo mengine ni ukosefu wa
miundombinu bora kama barabara za mitaani, ukosefu wa vyumba vya kutosha
vya madarasa, walimu wa kutosha hasa wa masomo ya sayansi na migogoro
ya ardhi kwenye maeneo mbalimbali.
ALISHINDA KWA MBINDE
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Mnyika alishinda kwa mbinde huku baadhi ya wapiga kura wake na wapambe wake, wakikesha nje kwa siku mbili kulinda kura zake kwa madai kwamba zilikuwa zikitaka kuchakachuliwa na ndiyo maana matokeo hayo yalicheleweshwa kutangazwa kwa siku tatu.

Awali, jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge Charles Keenja wa CCM na habari za chini kwa chini, zinaeleza kuwa kuna mikakati kabambe kutoka ndani ya chama hicho ya kuhakikisha jimbo hilo linarudi tena CCM.
“Kuna kila dalili Mheshimiwa Fenella
Mukangara akapitishwa na CCM kuchuana na Mnyika. Mnyika atatakiwa
kufanya kazi ya ziada kutetea jimbo lake,” kilisema chanzo chetu kwa
makubaliano ya kuhifadhi jina lake.
UPEPO WA KISIASA UPOJE?
Katika kunusanusa kwake, Uwazi Mizengwe ya Uchaguzi limebaini kwamba wananchi wa jimbo hilo wamegawanyika makundi mawili, wapo ambao wanaona Mnyika ameshindwa kuwasaidia hasa katika suala la maji na kutaka kubadilisha chama ingawa wapo wanaomuunga mkono kwamba ni mchapakazi mzuri.

MIZENGWE IMESHAANZA
“Japokuwa kampeni hazijaanza, kuna watu wa (anataja jina la chama) wanapita kwenye nyumba za watu na kuanza kumwaga sera ili muda wa uchaguzi ukifika tuwape kura. Wanagawa vyombo vya ndani vyenye nembo na rangi za chama yaani ni mizengwemitupu,” Mwantumu Hassan, mkazi wa Shekilango aliliambia Uwazi Mizengwe ya Uchaguzi.

Post a Comment