Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

TBC KUANZISHA KIPINDI CHA MAISHA YA WATANZANIA WALIO UGHAIBUNI

tiko tiko
Kaimu Mkurugenzi wa TBC ,Rosemary Jairo,  akizungumza jambo. 
Kulia ni Juma Hashim (kulia) na wa kwanza kushoto ni Edna Rajabu.Meneja Huduma wa TBC, Edna Rajabu,  akijibu maswali yaliyoulizwa na wanahabari.Mwasisi wa kipindi cha Bondeni,  Juma Hashim (katikati) akifafanua jambo.
Wanahabari wakifuatilia matukio ya hafla hiyo.
SHIRIKA la Utangazaji Tanzania (TBC) inatarajiwa kuwa na  kipindi cha kupitia televisheni (documentary) ambacho kitajulikana kama Bondeni. Akizungumza na wanahabari  leo jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Utangazaji TBC ,Rosemary Jairo, alisema kuwa kipindi hicho kitakuwa  cha kupitia televisheni (runinga) ya Tanzania iliyopo ughaibuni ambapo kitaonyesha  maisha ya kila siku ya Watanzania walioko nchi za nje  bila kujali uwezo  ama elimu waliyonayo.
Alisema kuwa kipindi hicho kimeanza kwa Watanzania waishio Afrika Kusini, nchi ambayo inaonekana kuongoza kwa kukaliwa na wageni wengi ambao sio wakimbizi,  wakiwemo vijana wa Kitanzania ambao wamekuwa wakimiminika kwa wingi nchini humo kwa lengo la kujipatia maisha bora zaidi.
Alisema pia vijana wengi wanakimbilia katika nchi hiyo kwa sababu  ina maendeleo  makubwa  kiuchumi ukilinganisha na nchi zingine za Afrika pia nchi hiyo inafikika kwa urahisi  kwa kupitia usafiri wa barabara.
Alitaja baadhi ya makundi ya kwanza ambayo yataanza kuonyeshwa katika kipindi hicho kuwa ni vijana wasiofanikiwa kimaisha na ukosefu wa elimu ya kutosha. 
Pia wataonyeshwa vijana ambao hawana vibali halali vya kuishi katika nchi hiyo, watu wenye mafanikio  na wanaomiliki miradi/biashara mbalimbali na jinsi wanavyoweza kuwasaidia ndugu zao waishio nchini Tanzania.
Pia wataonyeshwa wanafunzi ambao wapo ughaibuni kwa ajili ya kujiongezea elimu ya juu  kama vile shahada ya kwanza, uzamili na uzamivu, na hata kundi la viongozi wa serikali na mashirika ya umma wanaokwenda kwenye mikutano, warsha na semina.
Naye mwanzilishi wa kipindi hicho cha Bondeni, Juma Hashim Chillemba,  ambaye ni Mtanzania aishie nchini Afrika Kusini, alisema  kuna Watanzania wengi ambao wapo ughaibuni wakihangaika na kunyanyaswa, wengi wao wakihitaji msaada wa kurudi walikotoka.
Alisema  amefanya utafiti wa kutosha akiwa nchini Afrika Kusini na kuongea na vijana wa Tanzania na hata wa nchi nyingine na kuwapa elimu ya maisha ya ughaibuni, hivyo kuweza kuondoa dhana potofu kwamba wakati wote nje ya nchi maisha ni mazuri na rahisi kuyamudu,  jambo ambalo si kweli.
Hata hivyo,  alisema kuwa kipindi hicho kinatarajiwa badaye kutazamwa na kusikilizwa katika mataifa mengine yanayotumia lugha ya Kiswahili kama vile Burundi, Rwanda, Uganda,  Kenya  na hata Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Kipindi hicho kilichosajiliwa  hapa nyumbani na kupata ushirikiano  mkubwa wa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Radhia  Msuya,   kitasaidia kuwatafuta ndugu za Watanzania ughaibuni ili  kuwasiliana nao.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top