tiko
tiko
KAMA
mnavyofahamu, Chama cha Wazalendo ACT-Tanzania kitafanya mkutano wake
mkuu na uzinduzi wa chama mnamo tarehe 28 na 29 Machi 2015. Katika
mkutano Mkuu chama kitapitisha katiba mpya ya chama na kufanya uchaguzi
wa nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Kiongozi wa chama, Mwenyekiti wa
Chama, Makamu wenyeviti, Katibu Mkuu na Manaibu makatibu wakuu. Pia
chama kitachagua wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu.
Katika Uzinduzi wa chama tarehe 29 Machi 2015 kuanzia saa tisa alasiri,
viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wamealikwa. ACT – Tanzania
imemwalika Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, Mwenyekiti wa Taifa wa CUF
kuzungumza kwa niaba ya vyama vya upinzani nchini kuhusu ‘ kwanini
Tanzania bado ni nchi masikini na nini cha kufanya kuondoa umasikini’.
Pia viongozi wote wa vyama vya siasa nchini, mabalozi wa nchi mbalimbali
na wakuu wa asasi zisizo za kiserikali wamealikwa. Uzinduzi utaonyeshwa
moja kwa moja na vituo vya televisheni na radio kadhaa hapa nchini.
Mheshimiwa Samia Nkrumah, Kiongozi wa Chama cha CPP cha Ghana na mtoto
wa Rais wa kwanza wa Ghana Osagyefo Kwame Nkrumah amealikwa pamoja na
Mheshimiwa Ababu Namwamba, Katibu Mkuu wa chama cha ODM cha Kenya na
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Kenya.
Vile vile ACT – Tanzania inatarajiwa kupata wageni kutoka vyama rafiki
vya Ujerumani Die Linke na Umoja wa vyama vya mrengo wa kushoto
Progressive Alliance.
Baada ya Uzinduzi ACT Tanzania itafanya mikutano ya hadhara nchi nzima
kwa kuanzia na mikoa ya Arusha, Shinyanga, Tabora, Kigoma na Mbeya.
Jijini Arusha ACT – Tanzania itahuisha Azimio la Arusha na kuelezea
mwelekeo wa kisera wa chama katika kujenga Tanzania mpya yenye kufuata
misingi Usawa, Uzalendo, Uwazi, Uwajibikaji, Demokrasia na Uadilifu.
Imetolewa na:
Abdallah Khamis
Imetolewa na:
Abdallah Khamis
tiko
tiko
Post a Comment