tiko
tiko
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo akizungumza na kumpongeza
Doris Mollel wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo.
Meza kuu wakijianda kuelekea sehemu maalum ya kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo.
Mwenyekiti
wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel
ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel na
mshirika mwenza wa taasisi hiyo Heena Mujtaba kwa pamoja wakikata utepe
kuzindua taasisi yao huku Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo (kushoto) na Balozi Mwanaidi Sinare
wakishuhudia tukio hilo.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Balozi
Mwanaidi Sinare (kulia) akimpongeza Mwenyekiti wa taasisi
inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia
ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel kwenye uzinduzi huo.
Sehemu
ya ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria uzinduzi wa taasisi ya Doris
Mollel uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Hyatt Regency
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.
Meza kuu kwa pamoja wakikata cake maalum wakati wa uzinduzi huo.
Mwenyekiti
wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel
ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha
cake Balozi Mwanaidi Sinare.
Mwenyekiti
wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel
ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha
cake Muuguzi wa wodi ya watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mariana
Makanda (kushoto).
Mwenyekiti
wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel
ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha
kipande cha cake mshirika mwenza wa taasisi hiyo Heena Mujtaba.
Aliyekuwa
Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano
wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) akifurahia jambo
wakati wa uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel. Kulia ni Miss Tanzania
1998, Basila Mwanukuzi (kulia).
Mtangazaji wa kituo cha Channel Ten na Magic FM, Salma Msangi na rafiki yake wakati wa uzinduzi huo.
Mama
mzazi wa Doris Mollel , Bi. Celina Mollel (kushoto) katika picha ya
pamoja na wadau waliojitokeza kwenye uzinduzi wa taasisi ya Doris
Mollel. Kulia ni aliyekuwa Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa
Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu
pamoja na mfanyabiashara maarufu nchini, Bw. Ramesh Patel.
Mjasiriamali
Maznat Yusuph Sinare (aliyesimama katikati) akiteta jambo na Balozi
Mwanaidi Sinare (kulia) kwenye sherehe fupi za uzinduzi wa Doris Mollel
Foundation.
Balozi
Mwanaidi Sinare akisalimiana na Mh. Iddi Simba (aliyeipa mgongo kamera
yetu) Kulia ni mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mh. Mahmoud
Thabit Kombo.
Pichani
juu na chini ni Doris Mollel na familia yake akiwa kwenye picha ya
pamoja na wadau waliohudhuria uzinduzi wa taasisi yake.
Kutoka
kushoto ni Msanii wa filamu nchini, Sinta, Hoyce Temu pamoja na Rachel
Temu wakipiga picha kumbukumbu mara baada ya uzinduzi huo kufikia
tamati.
Na Mwandishi wetu
NAIBU Waziri wa Afya wa Serikali ya
Mapinduzi, Mahmoud Thabit Kombo ameitaka jamii kubadili utamaduni na
kumshikirisha mwanamme wakati mke wake akienda kujifungua ikiwa ni
sehemu ya kuhakikisha usalama wa mtoto na mama.
Alisema wanaume wengi hasa wanawake wao wanapokuwa wajawazito na wanakaribia kujifungua wanakosa amani na wengine hukimbia nyumbani au humkimbiza mke na mtoto wao kwa ndugu na jamaa baada ya kujifungua kutokana na kukosa ushauri unaompa ujasiri kuhusu familia yake hiyo mpya.
Naibu waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel mwishoni mwa wiki.
Alisema yeye anaamini kwamba moja ya vitu vinavyoweza kupunguza idadi ya vifo kwa watoto wa njiti ni ushiriki wa wanaume na kuwataka watu wa Doris Mollel Foundation kufanya kampeni kubwa ya kubadili tamaduni na wanaume kukalishwa chini kuelekezwa.
Aidha ushiriki wa wanaume katika ujauzito umeelezwa kusaidia kuondoa mashinikizo na ukosefu wa lishe bora kwa wawanake wajawazito kutokana na vitu hivyo kuwa sehemu ya uzazi wa watoto njiti.
Alisema pamoja na kutoa elimu kwa wanaume na wanawake hasa wauguzi juu ya haja ya wanaume kuona mahangaiko ya wanawake zao, ameitaka jamii kutambua kwamba uzazi katika umri mdogo ni tatizo jingine linalopsababisha uzazi wa watoto njiti.
Alisema kuhusu mabadiliko katika hospitali na zahanati zetu ili kuwa bora kwa uzazi salama Naibu waziri huyo alitaka taasisi mbalimbali kushirikiana na serikali kuhakikisha kwamba si watoto njiti tu wanakuwa salama bali hospitali na zahanati hizo zinakuwa salama kwa uzazi wa aina zote.
Awali wakati akimkaribisha Naibu Waziri kufungua taasisi hiyo, Balozi Mwanaidi Sinare, alisema kwamba ipo haja ya zahanati na hospitali za Tanzania zikawa katika hali ya kupokea uzazi wa aina zote ili watoto njiti waweze kuendelea kuishi.
Wakati huo huo mwasisi wa taasisi hiyo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wake, Doris Mollel ambaye ni Mrembo wa Singida 2014/15, ambaye alisema kwamba yeye alizaliwa akiwa njiti na uzito wa kilio 1.2 alisema zaidi ya watoto 200,000 huzaliwa njiti kila mwaka huku elfu 9 wakifariki.
Alisema wengi wa watoto hao hufariki kwa kukosa huduma muhimu hasa mashine za kuwawezesha kunyonya, kupata joto kuendelea kuishi kabla ya kutoka hospitalini.
Alisema lengo la kuanzisha taasisi hiyo ni kutafuta fedha za kuweza kusaidia watoto njiti ili kupunguza vifo na kuviondoa.
Watoto njiti milioni 15 huzaliwa duniani na kati yao milioni 1 hufa wengi wao kutoka nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania.

Post a Comment