tiko
tiko
Mechi hiyo iliyochezwa juzi ilimalizika
kwa ushindi wa bao 1-0 kwa Azam na kuendelea kukaa katika nafasi ya pili
kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 36 nyuma ya pointi moja
dhidi ya Yanga wenye 37.
Bao pekee la Azam lilifungwa na
mshambuliaji wao, John Bocco, na Kavumbagu alilazimika kutolewa nje huku
nafasi yake ikichukuliwa na Gaudence Mwaikimba.
Kavumbagu aliliambia gazeti hili kuwa
anaamini bado ana nafasi ya kufunga zaidi katika mechi zilizobaki lakini
kwa sasa anaangalia zaidi ushindi wa timu ili iweze kutetea ubingwa,
hivyo mchezaji yeyote atakayeifungia Azam hataweza kuharibu mahesabu
yake.
“Hii mechi tungepata mabao mengi ila
uwanja umetukwamisha sana, nafurahi timu yangu imeshinda japo kwa
ushindi wa bao moja, naamini nitafunga mechi zijazo na ninafurahi
mchezaji mwenzangu anapoifungia Azam kwani wote tupo kwa ajili ya
kufanikisha tunatetea ubingwa,” alisema Kavumbagu.
Kavumbagu ameshafunga mabao kumi akifuatiwa na Simon Msuva wa Yanga ambaye amefikisha mabao tisa.
Kocha Msaidizi wa Coastal Union, Jamhuri
Kihwelu ‘Julio’ amesikitishwa na timu yake kufungwa na mabingwa
watetezi, Azam FC, kitendo ambacho kimewadhalilisha kwa kile alichodai
kuwa wamefungwa na timu mbovu.
Coastal Union ilifungwa bao 1-0 na Azam juzi kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani.
Julio alisema anashangazwa na mpira wa
kiwango cha chini unaochezwa na Azam, ambayo ina kila kitu
kuanziamiundombinu na kuwalipa fedha nzuri wachezaji ambao yeye alidai
kuwa kiwango chao ni cha chini na hawapaswi kuwa hapo.
“Kinachoniuma ni kufungwa na timu mbovu
kama Azam, nashindwa kuelewa wachezaji wa Azam wana matatizo gani hadi
wanacheza kwa kiwango cha chini kiasi hiki, Azam ina kila kitu tofauti
na hizi timu zetu na kwa mfumo huu sidhani kama wanaweza kufika mbali
kisoka.
“Nafikiri hawana mipango mizuri katika
usajili ndiyo maana wachezaji waliopo wanashindwa kuipa hadhi klabu yao
kwa kuonyesha soka safi, tumefungwa ila wachezaji wangu wameonyesha
kiwango kizuri japokuwa nafasi walizozipata wameshindwa kuzitumia kama
wenzetu ambao wanabutua butua tu,” alisema Julio.
Kocha wa Azam, George Nsimbe alisema:
“Kwa sasa hatutaki kuangalia tunafunga mabao mangapi, kikubwa
tunachopigania ni kupata pointi tatu kila mechi na hii ni kutokana
kwamba tuna lengo la kutetea ubingwa, mechi zilizobaki tunatakiwa
kushinda zote.
tiko
tiko
Post a Comment