tiko
tiko
STAA wa
Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, ambaye anatumia dozi ya
kumwezesha kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, amesema kuwa mama yake
mzazi yu mgonjwa sana, akisumbuliwa na maumivu makali, Ijumaa Wikienda
lina mkasa kamili.
Mama mzazi wa Ray C, Margaret Mtweve.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa
wiki iliyopita, staa huyo alisema kwa zaidi ya siku tatu mfululizo, mama
yake alishindwa kupata usingizi kutokana na maumivu ya mifupa ya miguu
yaliyomfanya avimbe miguu, kitendo kilichosababisha ajikute akilia kama
mtoto mdogo.
“Ujue mara ya kwanza aliuguaga na
kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, baadaye Mungu alimjalia akapona
lakini naona ugonjwa wake umerudi tena. Anasumbuliwa na mifupa ambayo
inamfanya wakati mwingine avimbe miguu hadi anashindwa kutembea,”
alisema nyota huyo maarufu kama Kiuno Bila Mfupa.
Alisema mama yake amekuwa akipata shida
kutembea kiasi kwamba Ijumaa iliyopita, alimpeleka hospitali ya Wachina
iliyopo Sinza ili kupata vipimo na dawa, lakini haikusaidia.
“Hapa ninapoongea na wewe leo Jumamosi
Machi 14, nipo kwenye Hospitali ya Misheni hapa Tegeta tumekuja kupata
matibabu na kalazwa kwa muda ili afanyiwe vipimo vya MRI, maana leo
usiku hajalala kabisa kwani muda wote alikuwa akilalamika tu miguu
inamuuma.
“Imefikia wakati hadi nahisi maumivu
yake na nabaki nalia tu, nampenda sana mama yangu kiasi kwamba natamani
hata ningekuwa na fedha za kutosha kama zamani, hivi sasa ningekuwa nje
ya nchi kupata matibabu zaidi, anateseka usiku na mchana,” alisema Ray
C.
tiko
tiko
Post a Comment