tiko
tiko
Wabunge
wanaotoka mikoa ya mipakani wamelalamikia kuhusiana na watu wasio raia
kupiga kura na kuchaguliwa katika chaguzi kinyume cha sheria.
Wabunge hao ni Mbunge wa Viti Maalum, Josephine Genzabuke na Ally Keisy wote wa CCM walihoji juu ya tatizo hilo bungeni leo.
Katika swali lake la msingi Genzabuke
aliihoji serikali juu ya wakimbizi waliopiga kura katika baadhi ya
maeneo mkoani Kigoma ikizingatiwa ulikuwa uchaguzi wa serikali za mitaa
haukuwa na vitambulisho maalum kama vile kadi ya kupigia kura.
Swali lililoulizwa pia na Keissy ambaye
alisema katika jimbo lake kuna wenyeviti wa vijiji na vitongoji ambao
wamechaguliwa wakati si raia wa Tanzania?
Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri ofisi
ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa, Aggrey Mwanri
alisema serikali itakuwa tayari kushirikiana na mbunge ili kuchunguza
suala hilo na kuchukua hatua ya kulipatia ufumbuzi.
Hata hivyo, alisema ni jukumu la
viongozi wa vijiji, vitongoji na mitaa pamoja na wananchi kuwabaini watu
ambao siyo raia au wakazi wa eneo husika na kutoa taarifa kwa mamlaka
husika ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Alisema kwa mujibu wa kanuni kabla ya
siku ya uchaguzi orodha ya wapiga kura walioandikishwa hubandikwa katika
kituo cha kupigia kura ili kuwawezesha wananchi wa eneo husika kubaini
watu wasiokuwa na sifa wakiwemo wakimbizi au wasio wakazi wa eneo hilo
tiko
tiko
Post a Comment