tiko
tiko
Ndege
za kivita za muungano unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi la kigaidi
la Daesh nchini Syria zimefanya mashambulio katika maeneo kadhaa na
kuua raia 66 wa nchi hiyo. Harakati ya Kutetea Haki za Binadamu iliyoko
nchini Uingereza inayoitwa Syrian Observatory for Human Rights 'SOHM'
imeeleza kuwa, raia 66 wa Syria wakiwemo watoto 10 na wanawake 6
wameuawa katika mashambulio yaliyofanywa na ndege za kivita za muungano
ulioundwa na Marekani dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh katika mikoa ya
al Raqqa, Deir al Zor, al Hassakah, Idbil na mji wa Manjeb ulioko
umbali wa kilomita 446 kaskazini mwa Damascus, Mji mkuu wa Syria.
Muungano huo ulianza kufanya
mashambulizi ya anga tokea mwezi Septemba mwaka jana ndani ya ardhi za
Syria kwa kisingizio cha kushambulia ngome za kundi la kigaidi la Daesh,
ambalo limefanya unyama na mauaji makubwa nchini humo. Syria ilianza
kutumbukia kwenye ghasia na machafuko tokea mwezi Machi 2011, na hadi
sasa watu wasiopungua laki mbili na elfu kumi na tano wameshapoteza
maisha.
CHANZO: IRAN SWAHILI
tiko
tiko
Post a Comment