tiko
tiko
Marais
wa nchi sita za Afrika watakuwa na mkutano mkubwa leo Jijini Dar es
Salaam ncini Tanzania ambapo watajadili kwa kina juu ya kuboresha
uwekezaji katika kanda ya Maziwa Makuu. Marais hao ni Joseph Kabila wa
Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Pierre Nkurunziza wa Burundi, Paul
Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na
mwenyeji wao wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete.
Mkutano huo wa siku mbili utaambatana na
mdahalo baina ya viongozi hao na wadau mbalimbali katika sekta za
biashara na maendeleo. Mjadala wa viongozi hao utajikita katika umuhimu
wa Ukanda wa Kati ambao ni kiungo muhimu katika ukuaji uchumi wa nchi
hizo kwa kuwa husaidia katika uingizaji na uuzaji wa bidhaa mbalimbali
kupitia Tanzania kwa njia za maji, reli na barabara. Wakati wa mkutano
huo, viongozi hao watafanya uzinduzi wa treni ya mizigo kuelekea Uganda,
Rwanda na DRC.
CHANZO: IRAN SWAHILI REDIO
tiko
tiko
Post a Comment