tiko
tiko
BADO Mji wa Mafinga wilayani Mufindi
mkoani hapa haujakaa sawa kufuatia vifo vya watu 50 waliopoteza maisha
kwa ajali ya kontena kudondokea Basi la Majinja lenye namba za usajili T
438 CED iliyotokea Machi 11, 2015, Uwazi limechimba.
Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Changarawe
mjini Mafinga ambapo kontena hilo lilikuwa kwenye lori la mizigo la
Scania lenye namba za usajili T 689 APJ mali ya Kampuni ya Cipex
lililokuwa likitokea Dar kwenda Mbeya huku basi hilo likitokea Mbeya
kuelekea Dar.
KILICHOTOKEA BAADA YA AJALI
Kilichotokea baada ya ajali hiyo ni kuonekana kwa Mkono wa Mungu ambapo mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja mpaka miwili kunusurika katika ajali hiyo huku watu 50 wakipoteza maisha.
“Mimi naweza kusema ni Mkono wa Mungu kwa sababu, yule mtoto alikutwa hajaumia popote lakini wazazi wake wakiwa wamepoteza maisha. Huoni kama ni uwezo wa Mungu mwenyewe?” alisema askari polisi mmoja aliyekuwa miongoni mwa waliokuwa wakisimamia zoezi la uokoaji.

WAZAZI WA MTOTO
Akisimulia ilivyokuwa kwa wazazi wa mtoto huyo ambaye jina lake halijajulikana, mmoja wa abiria walionusurika, Aidan alisema kuwa, kabla ya kuanza safari jijini Mbeya, mtoto huyo alibebwa na mama yake akiwa ameongozana na abiria wengine.

“Wazazi wa mtoto waliingia na kukaa siti
ya tatu tu kutoka kwa dereva. Hakuna aliyehisi kwamba mbele ya safari
kuna janga kubwa kama hili.“Basi lilianza safari, kila abiria alikuwa
akizungumza na mwenzake, wengine walikuwa wakiongea na simu. Wapo
waliokuwa wakichati, nadhani ni wale wanaotumia WhatsApp. Kumbe bwana
shetani alikuwa anatembea na sisi,” alisema abiria huyo akiwa kwenye
Hospitali ya Wilaya ya Mufindi.
KABLA YA AJALI
Kwa mujibu wa majeruhi mwingine wa ajali hiyo, baada ya kufika eneo la Changarawe, kwa mbele lilionekana lori hilo likiwa katika mwendo wa kawaida na hakuna aliyewaza kwamba litaangukia basi lao.
Kwa mujibu wa majeruhi mwingine wa ajali hiyo, baada ya kufika eneo la Changarawe, kwa mbele lilionekana lori hilo likiwa katika mwendo wa kawaida na hakuna aliyewaza kwamba litaangukia basi lao.
“Mbele tuliliona lile lori likija,
lakini mimi nimekuwa nikisafiri mara kwa mara kwa kutumia barabara hiyo.
Najua eneo hilo lina shimo lakini sikuwa na wazo kwamba shimo lile
litakuwa mtoa roho wa abiria wa basi letu.
“Wakati tunapishana sasa, lori linapita kulia kwetu, mimi nilikaa siti ya nyuma upande wa abiria. Ghafla nilishtuka kuona kama giza linatanda upande wa dereva, mara nikasikia watu wakianza kulia.
“Wakati tunapishana sasa, lori linapita kulia kwetu, mimi nilikaa siti ya nyuma upande wa abiria. Ghafla nilishtuka kuona kama giza linatanda upande wa dereva, mara nikasikia watu wakianza kulia.
“Kabla sijajua ni nini, nikasikia
kishindo kikuu. Puuu! Abiria wengine walisikika wakisema wanakufa,
wengine wakiwa kimya! Ndipo nikajua tumeangukiwa na kontena lakini
sikuweza kufuatilia ilikuaje kwani akili zikawa kama zimeniruka,”
alisema abiria huyo bila kutaja jina lake.
KILICHOMTOKEA MTOTO HUYO
Baadhi ya waokoaji waliofika mapema mara baada ya ajali hiyo waliliambia Uwazi kwamba, wakati wanahangaika kuitoa miili ya majeruhi na marehemu, walishangaa kumkuta mtoto huyo akiwa chini ya siti ya nyuma kabisa maarufu kwa jina la ‘kwa balozi’, akiwa hana michubuko.

“Baadhi ya abiria walionusurika
wakatuambia huyu mtoto alikaa na wazazi wake kwenye siti ya tatu kutoka
kwa dereva. Sasa amefikaje kule nyuma kwa balozi? Nadhani anayejua ni
Mungu.“Unajua watoto wadogo wana mkono unaowalinda. Mara nyingi katika
ajali wao wanasalimika kwa njia ya ajabu sana,” alisema askari mmoja
wakati wa uokoaji.
Picha ya mtoto huyo ilipigwa na mpiga
picha Francis Godwin kwenye Wadi Namba 3 kwa kusaidiwa maelekezo na
polisi wa kike na muuguzi mmoja aliyekuwa na orodha ya watu
walionusurika. Watu wengine wawili kitandani hapo walikuwa ni wasamaria
wema waliokuwa wakimsaidia mtoto huyo ambapo wazazi wake wanasadikiwa
walipoteza maisha.
Polisi wakiwa eneo la tukio.
MGANGA MKUU NA MKUU WA MKOA
Juzi, Uwazi lilizungumza na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Salimin Mahimbo kuhusu ajali hiyo ambapo alisema mpaka sasa, majeruhi waliolazwa ni saba baada ya mmoja kufariki dunia na majeruhi mwingine kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutokana na hali yake kuzidi kuwa mbaya.

“Mpaka sasa tuna majeruhi saba tu, mmoja
alifariki dunia. Mmoja amekimbizwa Muhimbili kwa matibabu zaidi, hali
yake si nzuri, hawa saba wanaendelea vizuri,” alisema Mahimbo.Naye Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema mpaka juzi, marehemu wote
walishatambuliwa na ndugu zao na waliolazwa wametambuliwa pia.
tiko
tiko
Post a Comment