tiko
tiko
JESHI
la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limekanusha kuhusika kwa Idara
Usalama wa Taifa katika mipango ya kutaka kumuua Katibu mkuu wa chama
cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dokta Wilbroad Slaa.
Kauli
ya jeshi la polisi kanda hiyo ni kama inamjibu Mjumbe wa kamati kuu ya
CHADEMA (CC), Mabere Marando ambaye katika taarifa yake kwa vyombo vya
Habari alimtuhumu Naibu mkuu wa idara ya Usalama mkoa wa Kinondoni
Elisifa Ngowi kuandaa mipango miovu kwa dokta Slaa akishirikiana na
Mlinzi wa Katibu huyo bwana Khalid Kagenzi pamoja na Makumu mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Tanzania Bara,Philip Mangula.
Akikanusha
taarifa hizo leo Jijini Dar es Salaam,Kamishna wa Polisi Kanda maalum
ya Dar es Salaam,Suleiman Kova wakati na mkutano na vyombo vya Habari
amesema Jeshi hilo limefanya uchunguzi wakina ikiwemo kuchukua taarifa
upande wa chama cha Chadema na Mlinzi wa Dokta Slaa na kubaini hakuna
ukweli idara ya Usalama wa Taifa kuhusika.
“Tumefanya
uchunguzi wa kina ikiwemo kuwahoji watu wote wanaotuhumiwa .Tumebaini
kwa dhati kabisa hakuna mtu yeyote wa usalama wa Taifa aliyehusika
katika mipango ya kumdhuru Dokta Slaa", Amesema Kamishna Kova.
Kamishna
Kova ameongeza kuwa kwa sasa bado wanaendelea na uchunguzi wa suala
hilo na uchunguzi ukikamilika watafawakisha wahusika wote mahakamani
bila kumwogopa mtu yeyote.
Katika
hatua nyingine, Jeshi hilo linawashikiria watu wawili wanaojiita
viongozi wa watu waliopata mafunzo ya mgambo kwa kosa la kuratibu na
kuongoza vikao vya uchochezi vya mgambo dhidi ya serikali.
Kamishna
Kova amewataja watuhumiwa kwa majina kuwa ni Mathias lubega miaka
43,mkazi wa Bunju ambaye amekamatwa maeneo ya Mission Pup huko Mbagala
Mkoa wa Polisi Temeke.
Wa pili ni Mohamed Ally miaka 38 naye pia ni mkazi wa Mbagala .
Mbali
na kuwakamata watuhumiwa hao,kamishna Kova alithibitisha kuwa jeshi
hilo katika msako wake mkali limefanikiwa kukamata noti bandia za dolla
za kimarekani zipatazo 426 ambapo noti 36 ni za dolla 100 na noti 390
ni za dolla 50.
Kamishna
kova pia aliwataja kwa majina watuhumiwa ambao pesa hizo zilikutwa kwao
kuwa ni Ramadhani Mhambo miaka 34,mkazi wa Mwanayamala jijini Dr
,Eliazr Jackob Nkurarumi na Juma Mohamed mrundi miaka 25 ambaye ni
mlinzi wa Colombia Hoteli.
Mbali
na watuhumiwa hao, Kamishna Kova aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni
Rajabu Nassor miaka 30 ambaye ni fundi simu,Mkazi wa mwananyamala kwa
sindano ambapo wote wakuwa kwenye makazi yao walikutwa na fedha hizo
bandia.
tiko
tiko
Post a Comment