tiko
tiko
Kijana Paulo Ezekiel (kulia) akiwa kwenye mahojiano na mwandishi wa habari wamodewjiblog, Andrew Chale.
Mwandishi
wa habari wa modewjiblog, Andrew Chale (kushoto) akifanya mahojiano na
Paulo Ezekiel mara baada ya kukabidhi msaada wa baiskeli ya magudumu
matatu.
MO
DEWJI FOUNDATION: Ni taasisi iliyoanzishwa na Mbunge wa Singida Mjini
(CCM) na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji maarufu ‘MO’
(pichani) ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya kiongozi bora aliyejitolea
kwa kiasi kikubwa katika jamii na kuleta mabadiliko Afrika kwa mwaka
2014.
Taasisi
ya MO DEWJI FOUNDATION inayojishughulisha na miradi ya kusaidia jamii
Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo Afya, elimu na maji mwishoni
mwa wiki imeweza kumpatia kijana Paulo Ezekiel (23) msaada wa baiskeli
ya magurudumu matatu (tricycle) itakayomsaidia katika kutembelea kwenye
shughuli zake za kila siku.
Tukio
hilo la makabidhiano limefanyika katika ofisi za Mo Dewji Foundation
jijini Dar es Salaam ambapo Mtendaji Mkuu wa MO DEWJI FOUNDATION, Gerald
Mgesi David alikabidhi msaada huo kwa kijana Paulo Ezekieli
Akizungumza na Modewjiblog, Mtendaji
mkuu wa Mo Dewji Foundation amesema, waliguswa na usumbufu aliokuwa
anaupata kijana na hivyo kuona ni vyema kumsaidia ili aweze kumudu
kuendesha shughuli zake za kila siku.
Mo
Dewji Foundation imejikita katika kutekeleza miradi ya kijamii ambayo
inalenga kusaidia jamii ya kitanzania katika kujikwamua katika hali ya
umaskini na kuinua kipato.
Kwa
upande wake, kijana Paulo Ezekiel ambaye muda mfupi baada ya
kukabidhiwa baiskeli hiyo, alifanya mahojiano maalum na mtandao huu
ambapo alieza kuwa, tatizohilo la kulemaa mguu, lilimtokea ghafla wakati
yupo mitaa ya Kariakoo kwenye shughuli zake binafsi.
“Nakumbuka
nilikuwa kwenye matembezi maeneo ya Kariakoo, ghafla nilipata kuhisi
hali ya kupooza mguu mmoja wa kulia na kupoteza nguvu wasamaria wema
waliniokota na kunipeleka Muhimbili” anaeleza Paulo Ezekiel.
Alieleza kuwa, alikaa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa muda wa miezi sita huku akipatiwa matibabu na baadae aliruhusiwa.
“Niliporuhusiwa
hali ilikuwa ngumu sana. Kwani nilianza kuomba omba kwa watu msaada
ikiwemo kifaa cha kuniwezesha kunisaidia kutembelea. Kule Muhimbili
nilikuwa natumia baiskeli kutembelea hivyo nilivyoruhusiwa iliniwia
vigumu sana kutumia vifaa vya ulemavu ikiwemo haya magongo.
Kuna
siku katika kuomba omba. Nilikutana na mtu mmoja ambaye alinielekeza
kwa Mh. Dewji. Nilipofika kwake msaidizi wake alinitaka nifuatilia kuona
kama watafanikisha kwani tayari bajeti ilikuwa imeshafungwa hadi
kipindi kingine” alieleza Paulo Ezekiel.
Kijana
huyu awali alikua akifanya shughuli za kutafsiri Lugha kwa wageni
wanaokuja kununua bidhaa kwenye maduka ya Kariakoo na Bandari ya Dar es
Salaam hasa wafanyabiashara wanaotoka Congo, Rwanda, Zambia, Malawi,
Burundi na maeneo mbalimbali.
Paulo Ezekiel ni mtoto wa pili kati ya watoto nne, anatokea Mkoa wa Kilimanjaro na kabila lake ni Mchaga.
“Sikuamini
kama ningeweza kupata msaada huu. Hadi nilipofika hapa kukabidhiwa
namshukuru Mungu pia namuombea kwa Mungu Mh. Mohammed Dewji kwa msaada
wake, kwani simjui na wala hanijui..Ilikuwa ni kama bahati kufika katika
ofisi yake na kuomba msaada huu asante sana na namuombea maisha marefu
Dewji na familia yake, wafanyakazi wake wote popote pale kwani
kuniwezesha mimi ni ubinadamu mkubwa sana” alimalizia kijana Paulo
Ezekiel.
Paulo
Ezekiel anabainisha kuwa, ilikua vigumu sana kwa yeye kutembelea
magongo siku za mwanzoni ambapo anasema hakuwahi kutegemea kama siku
moja atakuja kuwa mlemavu.
“Hujafa,
hujaumbika naamini hilo, kwani awali nilikuwa najitafutia riziki zangu
za kujikimu kimaisha lakini nilipopata tatizo hili la kupooza mguu na
kulemaa ndoto zangu zote zimeyeyuka ila sijakata tama” Hivi ndivyo
anavyomalizia Paulo Ezekiel ambaye anaishi Mbagala, Temeke Jijini Dar es
Salaam, Tanzania.
Tuzo
hiyo aliyotunukiwa MO iitwayo African Philanthropist of the year Award
2014, Ilitolewa na jarida la uongozi la Uingereza, jijini Dubai wakati
wa Jukwaa la Viongozi wa Afrika.
Kabla
ya kukabidhiwa tuzo hiyo, sifa kuu aliyokuwa nayo MO kama alivyofafanua
wakati wa kukabidhiwa tuzo hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa jarida hilo, Dk
Ken Giami alisema wataalamu waelekezi walimchagua Dewji kuwa mshindi
kutokana na: Uongozi bora katika Kampuni yake ya Mohammed Enterprises
(MeTL GROUP) Pia kigezo kingine kilichompa ushindi ni namna
anavyojihusisha na kazi mbalimbali za kijamii.
Pia
Mchango wa MO katika elimu ni sehemu kubwa ya mafanikio yake hususan
kwa kuendeleza ujenzi wa shule mbili hadi 12, pamoja na kujitolea kiasi
cha zaidi ya Sh520 milioni katika kuendeleza sekta hiyo ya elimu ndani
ya jimbo lake hilo la Ubunge la Singida Mjini.
MO
pia amekuwa akisaidia sekta ya afya kwa ushirikiano na Taasisi ya Bilal
Muslim Mission ya Tanzania kwa kuwaleta madaktari waliowafanyia
upasuaji wagonjwa wa macho na 179 kupata miwani, kusambaza maji safi na
salama kwa kuchimba visima vingi vya maji ndani ya jimbo na n.k.
tiko
tiko
Post a Comment