tiko
tiko
VITENDO vya
ujambazi vinazidi kushika kasi kwenye jiji la Dar es Salaam, ambapo
tukio lingine limetokea leo mishale ya saa kumi jioni maeneo ya
Mikocheni Kwa-Mwalimu Nyerere baada ya watu wanne kutinga eneo hilo
wakiwa na pikipiki na kumpora mlinzi silaha aina ya Shot Gun aliyekuwa
akilinda kwenye ATM ya CRDB.
Majambazi hao waliitumia bunduki hiyo
kwa kuvamia duka la vinywaji lililokuwa jirani na kuiba kiasi kikubwa
cha pesa japo hakikuweza kufahamika kwa wakati huo.
Mtandao huu ulifanya juhudi za kumpata
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Kinondoni, Camillus Wambura ili kupata
undani wa tukio hilo na kiasi cha fedha kilichoibiwa ila simu yake ya
mkononi ilipokelewa na msaidizi wake aliyedai kuwa kamanda alikuwa
katika kikao.
tiko
tiko
Post a Comment