tiko
tiko
Bila shaka msomaji wangu unaendelea
vizuri na majukumu yako. Ni wiki nyingine tunapokutana tena kwenye
uwanja wetu huu. Wiki iliyopita tuliianza mada hii kama inavyojieleza
hapo juu.Tuliangalia mfano wa jinsi mwanaume mmoja ambaye yupo ndani ya
ndoa kwa kipindi cha miaka kumi lakini wazazi wake hawamtaki mkewe na
badala yake wamemtafutia mwanamke mwingine ambaye ndiyo wanamtaka.
ZUNGUMZA NA KILA UPANDE
Baada ya kufuata hatua ya kwanza ambayo nilisema ni kutafuta chanzo cha tatizo, hatua ya pili ni kuzungumza na kila upande. Ukishakijua chanzo, anza kuzungumza na mwenzi wako, mueleze jinsi unavyojisikia vibaya kutokana na uhasama uliopo kati yake na wazazi wako na mueleze msimamo wako.

Baada ya hapo, hamia upande wa pili,
zungumza na wazazi wako kwa heshima na uwaeleze jinsi unavyoumia
kutokana na matatizo yanayoendelea kati yao na mwenzi wako. Kamwe
usioneshe dharau kwao, zungumza nao kwa adabu huku ukiwapa heshima zote
wanazostahili kisha waeleze msimamo wako.
Kama kuna jambo aliwahi kuwaudhi ndiyo
maana hawamtaki na wanataka akawaombe msamaha, waahidi kwamba utasimamia
hilo hadi litimie ila kama wanataka muachane, nadhani huo hautakuwa
uamuzi sahihi, endelea kuzungumza nao mpaka muafaka upatikane.
WAPATANISHE
Baada ya kuwa umeshazungumza na pande zote mbili, andaa muda maalum ambao utawakutanisha wote, kama inawezekana unaweza pia kuwaita baadhi ya watu wachache unaowaamini kama washenga au viongozi wa dini waliofungisha ndoa yenu kisha kila mmoja azungumze dukuduku lake na mwisho, anayestahili kuomba radhi afanye hivyo.

Mpaka hapo tayari utakuwa umefanikisha
kupatikana kwa suluhu, busara kubwa itumike kuwapatanisha ili mkimaliza
kikao hicho cha suluhu, asiwepo ambaye bado atakuwa na dukuduku.
Baada ya kupatikana kwa suluhu, kuwa
makini ili yale yaliyosababisha matatizo awali, yasijirudie tena kwa
sababu wazazi wako hawawezi kumchukia tu mwenzi wako, lazima ipo sababu
ambayo unapaswa kuhakikisha kuwa baada ya muafaka, haijirudii
tena.Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri. Kwa maoni, ushauri,
nicheki kwa namba za hapo juu.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment