tiko
tiko
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Simon
Mwapagata ‘Rado’ amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya vibaka kukomba
vifaa vya gari lake vyenye thamani ya shilingi milioni tatu.
Akizungumza kwa huzuni juzikati, Rado
alisema siku ya tukio alipaki gari lake aina ya Toyota Mark X sehemu
aliyoizoea kila siku maeneo ya Mwananyamala na kwenda kulala lakini
alipoamka siku iliyofuata na kwenda kulichukua, alikuta site mirror, taa
zote, power window na vifaa vingine vimeibwa.
“Yaani nilihuzunika sana baada ya kukuta
gari langu liko kwenye hali hiyo huku mlinzi akiwa amelewa chakari
halafu hana hata shilingi useme labda anaweza kunilipa, nimeamua
kumwachia Mungu maana nikisema nikashtaki watakamatwa watu ambao ni
majirani zangu na mimi sitaki ugomvi nao,” alisema Rado.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment